Mwanzo / Kumbukumbu za habari
Kumbukumbu za habari

Sehemu hii inaonyesha habari za kumbukumbu pamoja na tarehe zake za awali za kuchapishwa. Habari imeonyeshwa katika lugha yake ya asili.

Uganda ipo tayari kuisaidia Israel vitani, asema Jenerali Muhoozi

Licha ya kutaka kukomeshwa kwa vita hivyo, Jenerali Muhoozi alisema kuwa Uganda itakuwa tayari kuisaidia Israel katika vita dhidi ya Iran. Mkuu wa Majeshi wa Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba amesema kuwa nchi yake ipo tayari kuisaidia Israel katika vita vya Mashariki ya Kati, iwapo taifa hilo...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Imesasishwa 13/8/2026, 05:26:22
Uganda ipo tayari kuisaidia Israel vitani, asema Jenerali Muhoozi
Kwa muhtasari

Licha ya kutaka kukomeshwa kwa vita hivyo, Jenerali Muhoozi alisema kuwa Uganda itakuwa tayari kuisaidia Israel katika vita dhidi ya Iran. Mkuu wa Majeshi wa Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba amesema kuwa nchi yake ipo tayari kuisaidia Israel katika vita vya Mashariki ya Kati, iwapo taifa hilo...

Licha ya kutaka kukomeshwa kwa vita hivyo, Jenerali Muhoozi alisema kuwa Uganda itakuwa tayari kuisaidia Israel katika vita dhidi ya Iran. Mkuu wa Majeshi wa Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba amesema kuwa nchi yake ipo tayari kuisaidia Israel katika vita vya Mashariki ya Kati, iwapo taifa hilo litashindwa. “Tunataka kuona vita vya Mashariki ya Kati vikiisha mara moja kwani dunia imeshachoka sasa. Hata hivyo, hatutosita kuingia vitani na kuisaidia Israel iwapo taifa hilo litaonekana kushindwa mapambano,” aliandika Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni, kupitia mtandao wa X, siku ya Jumatano. Kauli ya Jenerali Muhoozi inakuja huku vita vya Marekani-Israel dhidi ya Iran vikiendelea kupamba moto katika eneo la Mashariki ya Kati. Katika hatua nyingine, Kainerugaba ametangaza mpango wake wa kujenga sanamu ya Yonatan “Yoni” Netanyahu, ambaye ni ndugu yake Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ambaye aliuawa wakati wa harakati za kuwakomboa mateka katika uwanja wa ndege wa Entebbe, mwaka 1976. Chanzo: Newstimehub #Uganda #Israel #MuhooziKainerugaba #Jeshi #MsaadaWaKijeshi #SiasaZaKimataifa #MasharikiYaKati #MigogoroYaKikanda