الرئيسية / أرشيف الأخبار
أرشيف الأخبار

يعرض هذا القسم الأخبار المؤرشفة مع تواريخ نشرها الأصلية. يُعرض المقال بلغته الأصلية.

Kimbunga Gezani chaua takriban watu 59 Madagascar

Maelfu wamekosa makazi na mamia kujeruhiwa baada ya dhoruba kali kuikumba nchi hiyo ya visiwa vya Bahari ya Hindi. Takriban watu 59 wamepoteza maisha kufuatia athari za Kimbunga Gezani kilichoikumba Madagascar wiki iliyopita, kwa mujibu wa Ofisi ya Kitaifa ya Kudhibiti Hatari na Majanga (BNGRC)....

NewstimeTR Haber Merkezi · · آخر تحديث 13‏/8‏/2026، 5:26:23 ص
Kimbunga Gezani chaua takriban watu 59 Madagascar
لمحة سريعة

Maelfu wamekosa makazi na mamia kujeruhiwa baada ya dhoruba kali kuikumba nchi hiyo ya visiwa vya Bahari ya Hindi. Takriban watu 59 wamepoteza maisha kufuatia athari za Kimbunga Gezani kilichoikumba Madagascar wiki iliyopita, kwa mujibu wa Ofisi ya Kitaifa ya Kudhibiti Hatari na Majanga (BNGRC)....

Maelfu wamekosa makazi na mamia kujeruhiwa baada ya dhoruba kali kuikumba nchi hiyo ya visiwa vya Bahari ya Hindi. Takriban watu 59 wamepoteza maisha kufuatia athari za Kimbunga Gezani kilichoikumba Madagascar wiki iliyopita, kwa mujibu wa Ofisi ya Kitaifa ya Kudhibiti Hatari na Majanga (BNGRC). Watu 16,428 wamelazimika kuhama makazi yao, huku 15 wakiwa hawajulikani walipo na zaidi ya 800 wakijeruhiwa. Jumla ya watu 423,986 wameathiriwa na janga hilo. Gezani ilifika siku chache baada ya kimbunga kingine, Fytia, kilichoua watu 14 na kuwaacha zaidi ya 31,000 bila makazi. Katika kilele chake, Gezani ilikuwa na upepo mkali uliovuma hadi kilomita 270 kwa saa, uliosababisha uharibifu mkubwa wa nyumba na miundombinu. Baada ya kupita katika mkondo wa Msumbiji na kusababisha mawimbi makubwa, mfumo huo wa hali ya hewa umegeuza mwelekeo wake na unatabiriwa kurejea Madagascar. Mamlaka zimeiweka wilaya ya Ampanihy katika tahadhari huku zikihofia mafuriko mapya, ingawa mvua kubwa haitarajiwi. Chanzo: TRT Afrika #HaliYaHewa #MaafaYaAsili #KimbungaGezani #Madagascar #BahariYaHindi #BNGRC