Início / Arquivo de notícias
Arquivo de notícias

Esta secção apresenta notícias arquivadas com as datas de publicação originais. O artigo é apresentado no idioma original.

Watu 3 wafariki, na wengine wengi kuondoka katika makazi yao kutokana na mafuriko Nairobi, Kenya

Mwanamke mmoja, na watoto wake 2 walifariki baada ya kuangukiwa na ukuta wakati wa mvua kubwa Mvua kubwa ilionyesha katika mji mkuu wa Nairobi siku ya Jumanne imesababisha vifo vya watu watatu na wengine wengi wakiwa hawana makazi, polisi walisema. Mwanamke mmoja na watoto wake wawili walifariki...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Atualizado 13/08/2026, 05:26:23
Watu 3 wafariki, na wengine wengi kuondoka katika makazi yao kutokana na mafuriko Nairobi, Kenya
Em resumo

Mwanamke mmoja, na watoto wake 2 walifariki baada ya kuangukiwa na ukuta wakati wa mvua kubwa Mvua kubwa ilionyesha katika mji mkuu wa Nairobi siku ya Jumanne imesababisha vifo vya watu watatu na wengine wengi wakiwa hawana makazi, polisi walisema. Mwanamke mmoja na watoto wake wawili walifariki...

Mwanamke mmoja, na watoto wake 2 walifariki baada ya kuangukiwa na ukuta wakati wa mvua kubwa Mvua kubwa ilionyesha katika mji mkuu wa Nairobi siku ya Jumanne imesababisha vifo vya watu watatu na wengine wengi wakiwa hawana makazi, polisi walisema. Mwanamke mmoja na watoto wake wawili walifariki katika mtaa wa Mathare Phase 4 baada ya ukuta kuwaangukia nyumbani kwao wakati wa mvua kubwa. Polisi wanasema wawili hao walikufa papo hapo huku mmoja akifariki wakati akipelekwa hospitali. Familia zaidi ya 500 zimelazimika kuhama makazi yao katika mitaa ya mabanda, mamlaka zinasema. Maafisa wa huduma za dharura wamewataka wakazi kuchukua tahadhari huku Idara ya Hali ya Hewa nchini Kenya ikionya kuwa mvua hizi zitaendelea hadi 28 Aprili. Mkurugenzi wa idara hiyo Dkt. David Gikungu anasema mvua kubwa zinatarajiwa katika maeneo mbalimbali kote nchini. Wakazi wamesambaza video na picha katika mitandao ya kijamii zikionesha nyumba na magari yakisombwa na mafuriko. Watumiaji wengi wa mitandao wamelaumu serikali kwa kushindwa kuimarisha mifumo ya majitaka, wakiteta kuhusu kushindwa kutimiza ahadi walizotoa.