Mwanzo / Kumbukumbu za habari
Kumbukumbu za habari

Sehemu hii inaonyesha habari za kumbukumbu pamoja na tarehe zake za awali za kuchapishwa. Habari imeonyeshwa katika lugha yake ya asili.

Wataka uwajibikaji kwa familia zilizoathirika migodini

Wametaka kuwepo kwa kanuni madhubuti, ufuatiliaji huru na uwajibikaji zaidi kutoka kwa makampuni ya madini na serikali zinazotoa leseni. Wanaharakati wa mazingira chini ya bendera yao ya 'Indaba Mbadala ya Madini' waliandamana nje ya mkutano mkuu wa madini maarufu Indaba ya Madini huko Cape Town...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Imesasishwa 13/8/2026, 05:26:23
Wataka uwajibikaji kwa familia zilizoathirika migodini
Kwa muhtasari

Wametaka kuwepo kwa kanuni madhubuti, ufuatiliaji huru na uwajibikaji zaidi kutoka kwa makampuni ya madini na serikali zinazotoa leseni. Wanaharakati wa mazingira chini ya bendera yao ya 'Indaba Mbadala ya Madini' waliandamana nje ya mkutano mkuu wa madini maarufu Indaba ya Madini huko Cape Town...

Wametaka kuwepo kwa kanuni madhubuti, ufuatiliaji huru na uwajibikaji zaidi kutoka kwa makampuni ya madini na serikali zinazotoa leseni. Wanaharakati wa mazingira chini ya bendera yao ya 'Indaba Mbadala ya Madini' waliandamana nje ya mkutano mkuu wa madini maarufu Indaba ya Madini huko Cape Town nchini Afrika Kusini. Maandamano hayo yalifanyika Februari 11, 2026, ambapo wamezitaka serikali na makampuni ya uchimbaji madini kuchukua hatua zaidi ili kulinda jamii zilizoathirika na uchimbaji wa madini. Kundi hilo lilisema kuwa mkutano huo wa kila mwaka wa wadau wa madini na wawekezaji unaendelea kupuuza hasara za kimazingira na jamii zinazoathiriwa na shughuli zao kote barani Afrika. Wakati huo huo, walitaka kuwepo kwa kanuni madhubuti, ufuatiliaji huru na uwajibikaji zaidi kutoka kwa makampuni ya madini na serikali zinazotoa leseni. Indaba ya Madini ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya sekta ya madini barani Afrika, inayovutia wawekezaji wa kimataifa, wakati Indaba Mbadala ya Madini inajiweka kama jukwaa linalowakilisha sauti za wananchi.