Accueil / Archives
Archives

Cette rubrique présente les archives avec leurs dates de publication originales. L’article est affiché dans sa langue d’origine.

Wabunge wa Afrika Mashariki wapongeza ushindi wa Rais Samia

Pongezi hizo zinakuja wiki moja kabla ya wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hawajakutana jijini Nairobi. Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kufuatia ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Wakizungumza wakat...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Mis à jour 13/08/2026 05:26:23
Wabunge wa Afrika Mashariki wapongeza ushindi wa Rais Samia
En bref

Pongezi hizo zinakuja wiki moja kabla ya wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hawajakutana jijini Nairobi. Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kufuatia ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Wakizungumza wakat...

Pongezi hizo zinakuja wiki moja kabla ya wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hawajakutana jijini Nairobi. Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kufuatia ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Wakizungumza wakati wa kikao cha bunge hilo, kinachofanyika jijini Kampala Uganda, wajumbe hao walisema kuwa ushindi wa Samia ni dhihirisho la kielelezo cha mwanasiasa huyo, kuwa mfano kwa wanawake wengine barani Afrika na ulimwenguni kwa ujumla. “Amekuwa ni kielelezo na mfano kwa wanawake wengi duniani kwa kuwa kati ya wanawake wa kwanza barani Afrika kushika nafasi ya urais,” alisema Jacqueline Amongin mbunge wa EALA kutoka Uganda. Kauli hiyo iliungwa mkono na mbunge wa EALA kutoka Tanzania, Makame Hasnuu. “Hususani wanawake wanapozidi kung’aa katika nafasi za uongozi, hii inakuwa fahari na furaha kwa wanawake wote ambao ambao hawakuwahi kufikiria kushika nyadhifa ya juu kama ya urais,” alisema mbunge. Pongezi hizo zinakuja wiki moja kabla ya wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hawajakutana jijini Nairobi.