Ana Sayfa / Haber arşivi
Haber arşivi

Bu bölüm arşiv haberlerini özgün tarihleriyle gösterir. Haber metni özgün dilinde gösterilmektedir.

Waasi wa Sudan wametekeleza uhalifu dhidi ya binadamu katika mji wa El-Fasher - Umoja wa Mataifa

Uhalifu dhidi ya binadamu wa wapiganaji wa RSF ni pamoja na mauaji ya halaiki, dhulma za ngono, uporaji, na uharibifu wa maisha ya watu, wakati mwingine ikiwa pamoja na mateso na uangamizaji. Wapiganaji wa Rapid Support Forces wametekeleza uhalifu dhidi ya binadamu wakati wakizuia watu kuondoka E...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Güncellendi 13.08.2026 05:26:23
Waasi wa Sudan wametekeleza uhalifu dhidi ya binadamu katika mji wa El-Fasher - Umoja wa Mataifa
Bu haberde ne var?

Uhalifu dhidi ya binadamu wa wapiganaji wa RSF ni pamoja na mauaji ya halaiki, dhulma za ngono, uporaji, na uharibifu wa maisha ya watu, wakati mwingine ikiwa pamoja na mateso na uangamizaji. Wapiganaji wa Rapid Support Forces wametekeleza uhalifu dhidi ya binadamu wakati wakizuia watu kuondoka E...

Uhalifu dhidi ya binadamu wa wapiganaji wa RSF ni pamoja na mauaji ya halaiki, dhulma za ngono, uporaji, na uharibifu wa maisha ya watu, wakati mwingine ikiwa pamoja na mateso na uangamizaji. Wapiganaji wa Rapid Support Forces wametekeleza uhalifu dhidi ya binadamu wakati wakizuia watu kuondoka El-Fasher jimbo la magharibi mwa Sudan la Darfur, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulisema siku ya Ijumaa. Wanaotekeleza zaidi uovu huu ni RSF katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vinaingia mwaka wake wa tatu sasa, ujumbe huo ulisema kwenye ripoti yake ambayo ilisisitiza uchunguzi uliofanyika hapo awali. "RSF pia imefanya uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo mauaji ya watu wengi, dhulma za kingono, uporaji, na uharibifu wa maisha ya watu— wakati mwingine ikiwa ni pamoja na mateso na uangamizaji wa watu," mwenyekiti wa ujumbe, Mohamed Chande Othman, alisema katika taarifa. Kuzuia watu kutoka Kamati hiyo ya watu watatu ya Umoja wa Mataifa imepewa majukumu na Baraza la Haki la Binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza ukiukwaji huo wa haki.