Accueil / Archives
Archives

Cette rubrique présente les archives avec leurs dates de publication originales. L’article est affiché dans sa langue d’origine.

Waandamanaji nchini Madagascar wamtaka rais wa nchi hiyo ajiuzulu

Polisi wanatumia mabomu ya machozi, na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji. Takriban waandamanaji 1,000 waliandamana dhidi ya serikali katika mji mkuu wa Antananarivo nchini Madagascar, Alhamisi, wakimtaka Rais Andry Rajoelina ajiuzulu. Maandamano hayo yalifanyika wakati wa machafuko makubwa...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Mis à jour 13/08/2026 05:26:23
Waandamanaji nchini Madagascar wamtaka rais wa nchi hiyo ajiuzulu
En bref

Polisi wanatumia mabomu ya machozi, na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji. Takriban waandamanaji 1,000 waliandamana dhidi ya serikali katika mji mkuu wa Antananarivo nchini Madagascar, Alhamisi, wakimtaka Rais Andry Rajoelina ajiuzulu. Maandamano hayo yalifanyika wakati wa machafuko makubwa...

Polisi wanatumia mabomu ya machozi, na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji. Takriban waandamanaji 1,000 waliandamana dhidi ya serikali katika mji mkuu wa Antananarivo nchini Madagascar, Alhamisi, wakimtaka Rais Andry Rajoelina ajiuzulu. Maandamano hayo yalifanyika wakati wa machafuko makubwa zaidi kuwahi kufanyika nchini Madagascar, ambapo polisi walitumia mabomu ya machozi, na risasi za mpira kutawanya umati wa waandamanaji. Maandamano hayo, yanayoendeshwa na kizazi cha "Gen Z Madagascar," muungano wa wanafunzi na vijana, yalichochewa na hasira kutokana na kukatika kwa huduma za maji na umeme, lakini baadaye yaligeuka kuwa maandamano ya kumtaka Rais Rajoelina ajiuzulu. Hali hiyo ilizidi kuzorota, licha ya Rais Rajoelina kuvunja serikali yake na kuteua sura mpya katika baadhi ya wizara. SIku ya Jumatano, Rais Rajoelina alilaumu wale waliokuwa wakimtaka ajiuzulu kwa kutaka kuharibu nchi, huku akisema mbele ya mkutano kwenye ikulu kwamba atabadilisha hali ya nchi ndani ya mwaka mmoja. Mawakili wa waandamanaji walieleza waandishi wa habari kuwa wateja wao 28 wamepelekwa kwa ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka rasmi.