Ana Sayfa / Haber arşivi
Haber arşivi

Bu bölüm arşiv haberlerini özgün tarihleriyle gösterir. Haber metni özgün dilinde gösterilmektedir.

Mataifa 8 yakosoa uamuzi wa Israel kunyakua ardhi Ukingo wa Magharibi

Waziri wa mambo ya nje wa nchi nane wasema hatua hiyo ni kinyume cha sheria za kimataifa na inahatarisha suluhisho la mataifa mawili Mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Misri, Jordan, Indonesia, Pakistan, Qatar, Saudi Arabia na Falme za Kiarabu wamelaani vikali uamuzi wa Israel wa kutangaza maen...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Güncellendi 13.08.2026 05:26:23
Mataifa 8 yakosoa uamuzi wa Israel kunyakua ardhi Ukingo wa Magharibi
Bu haberde ne var?

Waziri wa mambo ya nje wa nchi nane wasema hatua hiyo ni kinyume cha sheria za kimataifa na inahatarisha suluhisho la mataifa mawili Mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Misri, Jordan, Indonesia, Pakistan, Qatar, Saudi Arabia na Falme za Kiarabu wamelaani vikali uamuzi wa Israel wa kutangaza maen...

Waziri wa mambo ya nje wa nchi nane wasema hatua hiyo ni kinyume cha sheria za kimataifa na inahatarisha suluhisho la mataifa mawili Mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Misri, Jordan, Indonesia, Pakistan, Qatar, Saudi Arabia na Falme za Kiarabu wamelaani vikali uamuzi wa Israel wa kutangaza maeneo makubwa ya Ukingo wa Magharibi kama “ardhi ya serikali.” Wamesema hatua hiyo ni ongezeko kubwa linalokiuka sheria za kimataifa na linaweza kuharakisha upanuzi wa makazi haramu pamoja na unyakuzi wa ardhi. Kwa mujibu wa tamko lao la pamoja, uamuzi huo unakiuka Mkataba wa Nne wa Geneva pamoja na Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 2334, linalotaka kusitishwa kwa ujenzi wa makazi ya walowezi. Pia umeelezwa kuwa kinyume na msimamo wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu mabadiliko ya hadhi ya maeneo yaliyokaliwa. Viongozi hao wameonya kuwa hatua hiyo inadhoofisha uwezekano wa suluhisho la mataifa mawili na inaweza kuongeza mvutano katika eneo hilo. Wameitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti kulinda haki za Wapalestina, ikiwemo haki ya kujitawala na kuanzishwa kwa taifa huru lenye mipaka ya mwaka 1967 na Yerusalemu Mashariki kuwa mji mkuu. Chanzo: TRT Afrika #Uturuki #Misri #Jordan #Indonesia #Pakistan #Qatar #SaudiArabia #UAE #Israel #UkingoWaMagharibi