Главная / Архив новостей
Архив новостей

В этом разделе представлены архивные новости с исходными датами публикации. Статья отображается на языке оригинала.

Uturuki kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya nchi tatu, Bosnia na Croatia katika mkutano wa ADF

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Fidan anatarajiwa kuonyesha wasi wasi wake kufuatia uamuzi dhidi ya Rais Milarad Dodi kwa Republika Srpska. Uturuki itakuwa mwenyeji wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi tatu ambazo ni Bosnia, Herzegovina na Croatia Aprili 12, 2025, pembezoni mwa Jukwaa la Kidiplo...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Обновлено 13.08.2026, 05:26:23
Uturuki kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya nchi tatu, Bosnia na Croatia katika mkutano wa ADF
Кратко

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Fidan anatarajiwa kuonyesha wasi wasi wake kufuatia uamuzi dhidi ya Rais Milarad Dodi kwa Republika Srpska. Uturuki itakuwa mwenyeji wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi tatu ambazo ni Bosnia, Herzegovina na Croatia Aprili 12, 2025, pembezoni mwa Jukwaa la Kidiplo...

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Fidan anatarajiwa kuonyesha wasi wasi wake kufuatia uamuzi dhidi ya Rais Milarad Dodi kwa Republika Srpska. Uturuki itakuwa mwenyeji wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi tatu ambazo ni Bosnia, Herzegovina na Croatia Aprili 12, 2025, pembezoni mwa Jukwaa la Kidiplomasia la Antalya (ADF). Mkutano wa Uturuki-Bosnia na Herzegovina-Croatia, utawaleta pamoja Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Bosnia na Herzegovina, na Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Ulaya Gordan Grlic Radman, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki. Majadiliano hayo yatajitika katika kuhakikisha utulivu Magharibi mwa Balkans, huku ikitilia mkazo kwa yanayojiri Bosnia na Herzegovina kufuatia hukumu ya hivi karibuni ya mahakama dhidi ya Milorad Dodik. Waziri Fidan anatarajiwa kusisitiza kwamba Uturuki inafuatilia kwa karibu na uungaji mkono wa Ankara kwa uhuru wa mipaka wa Bosnia na Herzegovina na ufuataji wa sheria, kutokana na Makubaliano ya Amani ya Dayton ya 1995. Pia ataelezea maoni ya hivi karibuni ya viongozi ya kutaka kujitenga kwamba hayakubaliki na kutilia mkazo wa umuhimu wa raia wa nchi hizo tatu katika kupunguza hali ya wasiwasi, kwa mujibu wa wizara. Fidan pia atatilia mkazo umuhimu wa uhusiano wa Bosnia, Herzegovin na Croatia katika kukuza amani ya muda mrefu katika kanda, imeongeza wizara. Mfumo wa mashauriano Mfumo wa Majadiliano wa nchi tatu umeundwa mwaka 2010, kwa lengo la kukuza ushirikiano wa kikanda na maendeleo. Mkusanyiko wa hivi sasa wa Antalya unakuwa mkutano wa kumi katika hatua ya wizara ya mambo ya nje, kufuatia mkutano uliopita ambao ulihodhiwa na Croatia, Dubrovnik Juni 2024. Katika wiki za hivi karibuni, Uturuki imeongeza jitihada za kidiplomasia kufuatia hali ya wasiwasi kutoka Republika Srpska. Rais Recep Tayyip Erdogan amekutana na Denis Bechirovic, mjumbe wa Baraza la Rais la Bosnia na Herzegovina, Machi 14 jijini Istanbul, akisisitiza nafasi ya Uturuki katika kuunga mkono uhuru wa nchi na mfumo wa katiba. Rais pia amefanya mazungumzo na mwenyekiti wa sasa na mjumbe wa Serb Jelka Cvijanovic Machi 22, katika mazungumzo ya simu tofauti na mjumbe wa Croatia Zeljko Komsic na kiongozi wa chama kikuu cha Bosnia SDA Bakir Izetbegovic. Uturuki, mjumbe wa kamati ya uendeshaji ya Baraza la Utekelezaji wa Amani wa Bosnia na Herzegovina, iko mbioni kuhakikisha amani na utulivu Bosnia na Herzegovina kupitia majukwaa ya kikanda na kimataifa. Uturuki ni nchi ambayo inachangia idadi kubwa ya vikosi kwa ujumbe wa amani wa kimataifa wa EUFOR-Althea Bosnia na Herzegovina, baada ya nchi wajumbe wa EU.