Ana Sayfa / Haber arşivi
Haber arşivi

Bu bölüm arşiv haberlerini özgün tarihleriyle gösterir. Haber metni özgün dilinde gösterilmektedir.

Uturuki inaongoza juhudi za kimataifa katika diplomasia ya kibinadamu na amani - Rais Erdogan

"Tunafanya juhudi kubwa kujenga nchi na eneo lisilo na ugaidi, ghasia," anasema Recep Tayyip Erdogan. Uturuki inaongoza juhudi za kimataifa katika diplomasia ya kibinadamu na amani, rais wa Uturuki amesema kufuatia mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine mjini Istanbul. Akizungumza katika ha...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Güncellendi 13.08.2026 05:26:23
Uturuki inaongoza juhudi za kimataifa katika diplomasia ya kibinadamu na amani - Rais Erdogan
Bu haberde ne var?

"Tunafanya juhudi kubwa kujenga nchi na eneo lisilo na ugaidi, ghasia," anasema Recep Tayyip Erdogan. Uturuki inaongoza juhudi za kimataifa katika diplomasia ya kibinadamu na amani, rais wa Uturuki amesema kufuatia mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine mjini Istanbul. Akizungumza katika ha...

"Tunafanya juhudi kubwa kujenga nchi na eneo lisilo na ugaidi, ghasia," anasema Recep Tayyip Erdogan. Uturuki inaongoza juhudi za kimataifa katika diplomasia ya kibinadamu na amani, rais wa Uturuki amesema kufuatia mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine mjini Istanbul. Akizungumza katika hafla iliyofanyika Istanbul siku ya Ijumaa, Recep Tayyip Erdogan alisema kuwa Uturuki ndiye "mchukuaji wa kiwango cha diplomasia ya kibinadamu" leo, akiongeza kuwa Uturukii "inaongoza diplomasia ya amani" kote ulimwenguni. Erdogan pia alisisitiza dhamira ya Uturuki ya kujenga eneo salama na lenye amani akisema: "Tunafanya juhudi kubwa kujenga nchi na eneo lisilo na ugaidi, ghasia na tishio la ugaidi." Mazungumzo ya amani ya Istanbul yaliyochukua takriban saa mbili yalihusisha maafisa wa ngazi ya juu wa kisiasa, ulinzi na kijasusi kutoka Urusi, Ukraine na Uturuki. Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov alithibitisha kuwa kila upande ulikubali kuwaachilia wafungwa 1,000, huku matarajio ya kusitisha mapigano pia yakijadiliwa. Ankara ilisisitiza jukumu lake kama mpatanishi, ikitoa wito wa maendeleo "kwenye njia ya amani."