Mwanzo / Kumbukumbu za habari
Kumbukumbu za habari

Sehemu hii inaonyesha habari za kumbukumbu pamoja na tarehe zake za awali za kuchapishwa. Habari imeonyeshwa katika lugha yake ya asili.

Umoja wa Mataifa washtumu mashambulizi ya ADF yaliyowaua raia 52 Mashariki mwa DRC

Mashambulizi hayo ‘ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za binaadamu za kimataifa,’ anasema mkuu wa MONUSCO Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) umeshtumu “vikali” mashambulizi yaliyofanywa na kundi la Allied Democratic Forces (ADF) ambayo yaliwaua raia wasiopungu...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Imesasishwa 13/8/2026, 05:26:22
Umoja wa Mataifa washtumu mashambulizi ya ADF yaliyowaua raia 52 Mashariki mwa DRC
Kwa muhtasari

Mashambulizi hayo ‘ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za binaadamu za kimataifa,’ anasema mkuu wa MONUSCO Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) umeshtumu “vikali” mashambulizi yaliyofanywa na kundi la Allied Democratic Forces (ADF) ambayo yaliwaua raia wasiopungu...

Mashambulizi hayo ‘ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za binaadamu za kimataifa,’ anasema mkuu wa MONUSCO Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) umeshtumu “vikali” mashambulizi yaliyofanywa na kundi la Allied Democratic Forces (ADF) ambayo yaliwaua raia wasiopungua 52 mashariki mwa nchi. ADF ililenga maeneo ya Beni na Lubero katika mkoa wa mashariki wa Kivu Kaskazini kuanzia Agosti 9 - 16 ikiwemo mauaji ya wanawake wanane na watoto wawili, taarifa ya MONUSCO ilisema siku ya Jumatatu. Bintou Keita, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Congo na kiongozi wa MONUSCO, anasema mashambulizi, yanakuja baada ya mashambulizi ya ADF katika kanisa moja mwishoni mwa mwezi Julai, ambayo yalikuwa “ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za binaadamu za kimataifa,.”