Wachezaji hao wameadhibiwa kutokana na ishara zao walizozionesha wakati wa kushangilia kwenye mchezo wao dhidi ya Atletico Madrid katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kylian Mbappe na Antonio Rudiger watakosa mchezo mmoja kila moja, kufuatia adhabu waliyopewa na Kamati ya Usimamizi wa Maadili na Nidhamu ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA). Wakati huo huo, Rudiger ametozwa faini ya Dola za Kimarekani 43,738 huku nyota wa Ufaransa Mbappe akitakiwa kulipa dola 33,000, pamoja na kulazimika kukosa mchezo mmoja kwa “utovu wa nidhamu na kukiuka kanuni za uungwana michezoni,” kulingana na taarifa ya UEFA iliyotolewa siku ya Ijumaa. Mbali na adhabu hizo, wachezaji hao watakuwa chini ya usimamizi kwa kipindi cha mwaka mmoja, UEFA iliongeza. Kwa upande wake, mchezaji mwingine wa vigogo hao wa soka barani Ulaya, Daniel Ceballos, alitozwa faini ya dola 22,000, japo hakusimamishwa kushiriki mchezo mmoja kama ilivyo kwa wenzake. Katika mchezo huo uliofanyika Machi 12, 2025, Real Madrid iliishinda Atletico Madrid kwa njia ya ‘matuta’, katika mchezo wa pili wa hatua ya mtoano uliofanyika katika uwanja wa Wanda Metropolitano jijini Madrid.
Cette rubrique présente les archives avec leurs dates de publication originales. L’article est affiché dans sa langue d’origine.
UEFA yawapiga faini Kylian Mbappe na Antonio Rudiger
Wachezaji hao wameadhibiwa kutokana na ishara zao walizozionesha wakati wa kushangilia kwenye mchezo wao dhidi ya Atletico Madrid katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kylian Mbappe na Antonio Rudiger watakosa mchezo mmoja kila moja, kufuatia adhabu waliyopewa na Kamati ya Usimamizi w...