“Nina uhusiano mzuri sana, sana na Uturuki na kiongozi wake,” amesema Rais wa Marekani Trump mapema wiki hii. Rais wa Marekani Donald Trump anafikiria kuiongeza Uturuki katika ziara yake ya Mashariki ya Kati iliyopangwa mwezi ujao, imeripoti CCN Arabic. Ziara hiyo itakuja baada ya Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu, hayo ni kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa White House na vyanzo vyengine viwili ambavyo vina taarifa ya safari hiyo. Hakuna uamuzi uliofanyika, na taarifa zaidi ziko katika hatua ya mwisho, vimesema vyanzo hivyo. Uhusiano mzuri na Uturuki Afisa mwandamizi wa Ikulu ya White House amekiambia kituo hicho cha habari kwamba Trump amejadili kuhusu safari hiyo katika mazungumzo yake ya hivi karibuni na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Rais wa Marekani hana mpango wa kuitembelea Israeli katika ziara hiyo, kwa mujibu wa vyanzo. Ikulu ya White House haikutoa ufafanuzi wa haraka kwa Shirika la Anadolu pindi lilipotaka ufafanuzi. Trump awali alielezea uhusiano wake mzuri aliokuwa nao na Erdogan. “Nina uhusiano mzuri sana, sana na Uturuki na kiongozi wao,” Trump alisema mwanzoni mwa wiki hii, akiwa na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu White House. “Amemuelezea Erdogan kama “mtu mwenye nguvu na mwerevu, na amefanya kitu ambacho hakuna mtu aliweza kukifanya,” akiashiria kwamba, anaamini “ni Uturuki” iliyosuka mpango wa kuuangusha utawala wa Syria wa Bashar al Assad. Iwapo safari hiyo itafanikiwa, itakuwa safari ya Trump ya kwanza kama rais nchini Uturuki. Watangulizi wake George W. Bush aliitembelea mwaka 2004, huku Barack Obama aliitembelea mwaka 2009 na 2015.
Cette rubrique présente les archives avec leurs dates de publication originales. L’article est affiché dans sa langue d’origine.
Trump apanga safari ya Uturuki kama sehemu ya ziara yake Mashariki ya Kati: Ripoti
“Nina uhusiano mzuri sana, sana na Uturuki na kiongozi wake,” amesema Rais wa Marekani Trump mapema wiki hii. Rais wa Marekani Donald Trump anafikiria kuiongeza Uturuki katika ziara yake ya Mashariki ya Kati iliyopangwa mwezi ujao, imeripoti CCN Arabic. Ziara hiyo itakuja baada ya Saudi Arabia, Q...
“Nina uhusiano mzuri sana, sana na Uturuki na kiongozi wake,” amesema Rais wa Marekani Trump mapema wiki hii. Rais wa Marekani Donald Trump anafikiria kuiongeza Uturuki katika ziara yake ya Mashariki ya Kati iliyopangwa mwezi ujao, imeripoti CCN Arabic. Ziara hiyo itakuja baada ya Saudi Arabia, Q...
