Gida / Taskar labarai
Taskar labarai

Wannan sashe yana nuna tsoffin labarai da ranakun da aka wallafa su. An nuna labarin a harshensa na asali.

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.2 lapiga Istanbul, hakuna madhara yaliyoripotiwa

Tetemeko la ardhi Istanbul. Nawatakia mema raia wetu, na tunafuatilia kwa karibu yanayojiri, amesema Rais Recep Tayyip Erdogan Tetemeko lenye ukubwa wa 6.2 limepiga Uturuki, huku kitovu kikiwa wilaya ya Silivri iliyopo Istanbul, kwa mujibu wa Kitengo cha Maafa na Dharura cha Uturuki (AFAD). Tetem...

NewstimeTR Haber Merkezi · · An sabunta 2026-08-13, 05:26:21
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.2 lapiga Istanbul, hakuna madhara yaliyoripotiwa
A taƙaice

Tetemeko la ardhi Istanbul. Nawatakia mema raia wetu, na tunafuatilia kwa karibu yanayojiri, amesema Rais Recep Tayyip Erdogan Tetemeko lenye ukubwa wa 6.2 limepiga Uturuki, huku kitovu kikiwa wilaya ya Silivri iliyopo Istanbul, kwa mujibu wa Kitengo cha Maafa na Dharura cha Uturuki (AFAD). Tetem...

Tetemeko la ardhi Istanbul. Nawatakia mema raia wetu, na tunafuatilia kwa karibu yanayojiri, amesema Rais Recep Tayyip Erdogan Tetemeko lenye ukubwa wa 6.2 limepiga Uturuki, huku kitovu kikiwa wilaya ya Silivri iliyopo Istanbul, kwa mujibu wa Kitengo cha Maafa na Dharura cha Uturuki (AFAD). Tetemeko hilo limepiga majira ya saa 6:49 muda wa Istanbul na kusikika zaidi Istanbul siku ya Jumatano na mikoa jirani, hivyo kusababisha wakazi kutoka majumbani kwa hofu. Tetemeko jengine lenye ukubwa wa 4.9 limepiga saa 7.02 mchana, huku likisikika zaidi katika pwani ya Buyukcekmece katika Bahari ya Marmara. AFAD imesema taasisi husika ziko katika tahadhari na tathmini inafanyika kubaini uharibifu na kuhakikisha usalama wa raia. AFAD imesisitiza kuwa vikosi vinafuatilia na kuratibu jitihada za mwitikio. Mpaka sasa hakuna taarifa za madhara au uharibifu mkubwa. Katika taarifa, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema mamlaka inafuatilia kwa karibu yanayojiri.