Home / News archive
News archive

This section shows archived news with its original publication dates. The article is displayed in its original language.

Tanzania yamuachilia Agather, mwanaharakati wa Uganda

Agather Atuhaire alikamatwa pamoja na mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi walipokuwa wameenda nchini humo kushuhudia kesi ya mwanasiasa wa upinzani Tanzania, Tundu lissu. Mwandishi wa habari wa Uganda na mwanaharakati wa haki za binadamu Agather Atuhaire amepatikana akiwa hai baada ya siku kad...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Updated 13/08/2026, 05:26:21
Tanzania yamuachilia Agather, mwanaharakati wa Uganda
At a glance

Agather Atuhaire alikamatwa pamoja na mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi walipokuwa wameenda nchini humo kushuhudia kesi ya mwanasiasa wa upinzani Tanzania, Tundu lissu. Mwandishi wa habari wa Uganda na mwanaharakati wa haki za binadamu Agather Atuhaire amepatikana akiwa hai baada ya siku kad...

Agather Atuhaire alikamatwa pamoja na mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi walipokuwa wameenda nchini humo kushuhudia kesi ya mwanasiasa wa upinzani Tanzania, Tundu lissu. Mwandishi wa habari wa Uganda na mwanaharakati wa haki za binadamu Agather Atuhaire amepatikana akiwa hai baada ya siku kadhaa za kuzuiliwa nchini Tanzania bila mawasiliano. Vyanzo vya habari nchini Uganda vinathibitisha kwamba alipatikana katika mpaka wa Uganda na Tanzania huko Mutukula Alhamisi usiku, akiwa katika hali mbaya na bila kuwepo na taarifa rasmi ya kuachiliwa kwake. Atuhaire, ambaye alikamatwa Mei 19 jijini Dar es Salaam, hivi sasa yuko chini ya uangalizi wa marafiki na jamaa wanaomsaidia kurejea Kampala. Kuachliwa kwake kunafuatia jitihada za ubalozi wa Uganda nchini Tanzanai kuiandikia serikali ya Tanzania rasmi huku ikiomba Agather aweze kutembelewa na maafisa wa ubalozi. Agather amaeachiliwa baada ya mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi pia kuachiliwa.