Kwa sasa, Simba ambayo inasuburi kumjua mpinzani wake kwenye hatua inayofuata, ndiye muwakilishi pekee kwenye michuano ya kimataifa kutoka ukanda wa Afrika Mashariki. Klabu ya Soka ya Tanzania, Simba Sports Club imesonga mbele kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga Al Masry kwa mikwaju 4-1. Katika mchezo huo wa pili wa hatua ya robo fainali uliofanyika Aprili 9, 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Simba ilishinda kwa mabao 2-0, yaliyofungwa na Elia Mpanzu katika dakika ya 20, likifuatiwa na bao lililotiwa kimiani na Steven Mukwala katika dakika ya 50 ya mchezo, na hivyo kufanya matokeo yawe 2-2, baada ya Al Masry kushinda mchezo wao wa awali. Hata hivyo Simba iliibuka ‘kidedea’ katika hatua za penati, baada kushinda penati 4 dhidi ya 1 kutoka kwa Al Masry, na hivyo kuifanya isonge mbele kwenye hatua inayofuata ya Kombe le Shirikisho la CAF. Ulikuwa ni uhodari wa Moussa Camara maarufu kama ‘Spider Man’, aliyeokoa michomo miwili ya penati za Wamisri. Kwa sasa, Simba ambayo inasuburi kumjua mpinzani wake kwenye hatua inayofuata, ndiye muwakilishi pekee kwenye michuano ya kimataifa kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.
Cette rubrique présente les archives avec leurs dates de publication originales. L’article est affiché dans sa langue d’origine.
Tanzania: Simba Sports Club yatinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF
Kwa sasa, Simba ambayo inasuburi kumjua mpinzani wake kwenye hatua inayofuata, ndiye muwakilishi pekee kwenye michuano ya kimataifa kutoka ukanda wa Afrika Mashariki. Klabu ya Soka ya Tanzania, Simba Sports Club imesonga mbele kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga Al Masry kwa...