Accueil / Archives
Archives

Cette rubrique présente les archives avec leurs dates de publication originales. L’article est affiché dans sa langue d’origine.

Sudan yasitisha uhusiano wa kidiplomasia na UAE

Sudan imeitaja UAE kama ‘taifa la uchokozi,’ huku taifa hilo la Ghuba likikanusha madai ya kuwaunga mkono wapiganaji wa RSF Siku ya Jumanne Sudan imesitisha ushirikiano wa kidiplomasia na UAE na kumrejesha nyumbani balozi wake kutoka Abu Dhabi. Katika taarifa, Baraza la Usalama na Ulinzi la Sudan...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Mis à jour 13/08/2026 05:26:21
Sudan yasitisha uhusiano wa kidiplomasia na UAE
En bref

Sudan imeitaja UAE kama ‘taifa la uchokozi,’ huku taifa hilo la Ghuba likikanusha madai ya kuwaunga mkono wapiganaji wa RSF Siku ya Jumanne Sudan imesitisha ushirikiano wa kidiplomasia na UAE na kumrejesha nyumbani balozi wake kutoka Abu Dhabi. Katika taarifa, Baraza la Usalama na Ulinzi la Sudan...

Sudan imeitaja UAE kama ‘taifa la uchokozi,’ huku taifa hilo la Ghuba likikanusha madai ya kuwaunga mkono wapiganaji wa RSF Siku ya Jumanne Sudan imesitisha ushirikiano wa kidiplomasia na UAE na kumrejesha nyumbani balozi wake kutoka Abu Dhabi. Katika taarifa, Baraza la Usalama na Ulinzi la Sudan limeitaja UAE kama “taifa la uchokozi,” na kuishtumu nchi hiyo ya Ghuba kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa RSF. “Dunia nzima imeshuhudia, kwa zaidi ya miaka miwili, UAE imefanya uhalifu dhidi ya uhuru wa Sudan, na mipaka yake, na usalama wa raia wake,” baraza hilo limesema. Uamuzi huo umekuja siku moja baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuitupilia mbali kesi ya Sudan ya kudai kuwa UAE “inahusika na mauaji ya halaiki” katika mkoa wa Darfur magharibi kutokana madai ya kuwasaidia RSF, madai ambayo UAE inakanusha. UAE haijasema chochote kuhusu uamuzi huo wa Sudan. ​​​​​​​