Ana Sayfa / Haber arşivi
Haber arşivi

Bu bölüm arşiv haberlerini özgün tarihleriyle gösterir. Haber metni özgün dilinde gösterilmektedir.

Somalia kuanza kutoa pasipoti za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa raia wake

Hatua hiyo inalenga kurahisisha usafiri na kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika Afrika Mashariki. Somalia inatarajiwa kuanza kutoa pasipoti za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa raia wake, ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kurahisisha uhuru wa kusafiri ndani ya...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Güncellendi 13.08.2026 05:26:20
Somalia kuanza kutoa pasipoti za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa raia wake
Bu haberde ne var?

Hatua hiyo inalenga kurahisisha usafiri na kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika Afrika Mashariki. Somalia inatarajiwa kuanza kutoa pasipoti za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa raia wake, ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kurahisisha uhuru wa kusafiri ndani ya...

Hatua hiyo inalenga kurahisisha usafiri na kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika Afrika Mashariki. Somalia inatarajiwa kuanza kutoa pasipoti za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa raia wake, ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kurahisisha uhuru wa kusafiri ndani ya Afrika Mashariki. Balozi wa Somalia nchini Tanzania, Ilyas Ali Hassan, aliwasilisha rasmi mfano wa pasipoti hiyo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Somalia, Jenerali Abdullahi Sheikh Ismail “Fartaag”, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Uhamiaji, Mustafa Sheikh Ahmed Dhuhulow. Somalia iliidhinishwa kuchapisha pasipoti hizo mwezi Desemba 2025, na muundo rasmi ulitangazwa hivi karibuni. Pasipoti za EAC zilianzishwa mwaka 2016 na zinapatikana katika madaraja matatu: za kidiplomasia, za watumishi wa umma na za kawaida, zikiwa na mfumo wa kielektroniki unaotambulika kimataifa. Somalia iliingia rasmi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2024 kama mwanachama wa nane, na tayari imeteua wawakilishi wake katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA). Nchi nyingine wanachama wa EAC ni pamoja na Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Chanzo: TRT Afrika #Usafiri #Diplomasia #Ushirikiano #Pasipoti #AfrikaMashariki #EAC #Somalia #Tanzania