Accueil / Archives
Archives

Cette rubrique présente les archives avec leurs dates de publication originales. L’article est affiché dans sa langue d’origine.

Shadrack Maluki rais mpya wa Kamati ya Olimpiki Kenya

Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Judo nchini Kenya, Shadrack Maluki, ndiye rais mpya wa Kamati ya Olimpiki nchini Kenya. Maluki alimshinda katibu mkuu anayeondoka Francis Mutuku katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumatatu. Maluki, ambaye alikuwa makamu wa kwanza wa Kamati ya Olimpiki, alipata k...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Mis à jour 13/08/2026 05:26:20
Shadrack Maluki rais mpya wa Kamati ya Olimpiki Kenya
En bref

Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Judo nchini Kenya, Shadrack Maluki, ndiye rais mpya wa Kamati ya Olimpiki nchini Kenya. Maluki alimshinda katibu mkuu anayeondoka Francis Mutuku katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumatatu. Maluki, ambaye alikuwa makamu wa kwanza wa Kamati ya Olimpiki, alipata k...

Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Judo nchini Kenya, Shadrack Maluki, ndiye rais mpya wa Kamati ya Olimpiki nchini Kenya. Maluki alimshinda katibu mkuu anayeondoka Francis Mutuku katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumatatu. Maluki, ambaye alikuwa makamu wa kwanza wa Kamati ya Olimpiki, alipata kura 15 kutoka kwa mashirikisho 27 yaliyowakilishwa, huku Mutuku, akifanikiwa kupata kura 12. Shadrack anachukua nafasi ya Paul Tergat, mwanariadha mstaafu wa mbio za masafa marefu ambaye amemaliza muda wake. Maluki pamoja na maafisa wengine wa nyadhifa mbalimbali kwenye kamati yake wanatarajiwa kusimamia maandalizi ya Olimpiki ijayo, hasa wakizingatia kuimarisha wanamichezo, uwazi, na matokeo ya Kenya katika michezo hiyo ulimwenguni.