Rais Andry Rajoelina amekiri kuwa "waziri wa nishati hakuwa anafanya kazi yake kama inavyotakiwa". Siku ya Ijumaa rais wa Madagascar amemfuta kazi waziri wake wa nishati kwa lengo la kutuliza maandamano kuhusu kukatwa kwa umeme mara kwa mara na uhaba wa maji, ambayo yamesababisha machafuko katika mjii mkuu siku moja kabla. Polisi walitumia risasi za mpira na mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji wengi wao wakiwa vijana katika mji wa Antananarivo siku ya Alhamisi, katika maandamano ambayo Rais Andry Rajoelina ameyaita "ya kutatiza nchi sawa na mapinduzi" katika kauli yake ya kwanza kwa njia ya video. Walioandaa maandamano siku ya Ijumaa walitaka watu ambao hawaridhiki na serikali ya Rajoelina "kujitokeza kwa wingi" kwa "maandamano ya amani" siku ya Jumamosi asubuhi, wakijitenga na matukio ya uporaji ya siku ya Alhamisi.
Taskar labarai
Wannan sashe yana nuna tsoffin labarai da ranakun da aka wallafa su. An nuna labarin a harshensa na asali.
Rais wa Madagascar amfuta kazi waziri wa nishati baada ya maandamano kuhusu kukatwa kwa umeme
Rais Andry Rajoelina amekiri kuwa "waziri wa nishati hakuwa anafanya kazi yake kama inavyotakiwa". Siku ya Ijumaa rais wa Madagascar amemfuta kazi waziri wake wa nishati kwa lengo la kutuliza maandamano kuhusu kukatwa kwa umeme mara kwa mara na uhaba wa maji, ambayo yamesababisha machafuko katika...
A taƙaice