Ana Sayfa / Haber arşivi
Haber arşivi

Bu bölüm arşiv haberlerini özgün tarihleriyle gösterir. Haber metni özgün dilinde gösterilmektedir.

Rais wa Ghana Mahama amsimamisha kazi Jaji Mkuu

Kumewasilishwa malalamiko rasmi matatu kutaka aondolewe ofisini, hata hivyo madai dhidi yake hayajafahamika wazi kwa umma. Siku ya Jumanne rais wa Ghana John Dramani Mahama amemsimamisha kazi Jaji Mkuu wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi wakisubiri matokeo ya uchunguzi dhidi yake, taarifa ilisema. J...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Güncellendi 13.08.2026 05:26:19
Rais wa Ghana Mahama amsimamisha kazi Jaji Mkuu
Bu haberde ne var?

Kumewasilishwa malalamiko rasmi matatu kutaka aondolewe ofisini, hata hivyo madai dhidi yake hayajafahamika wazi kwa umma. Siku ya Jumanne rais wa Ghana John Dramani Mahama amemsimamisha kazi Jaji Mkuu wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi wakisubiri matokeo ya uchunguzi dhidi yake, taarifa ilisema. J...

Kumewasilishwa malalamiko rasmi matatu kutaka aondolewe ofisini, hata hivyo madai dhidi yake hayajafahamika wazi kwa umma. Siku ya Jumanne rais wa Ghana John Dramani Mahama amemsimamisha kazi Jaji Mkuu wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi wakisubiri matokeo ya uchunguzi dhidi yake, taarifa ilisema. Jaji Gertrude Torkornoo aliapishwa kuwa Jaji Mkuu Juni 2023. Aliongoza hafla ya kuapishwa kwa Rais Mahama kwa muhula wake wa pili mwezi Januari . Malalamiko rasmi matatu yamewasilishwa kutaka aondolewe ofisini.Hata hivyo madai dhidi yake hayajafahamika wazi kwa umma. Rais Mahama ana sababu za kuamini kuwepo kwa ushahidi wa kutosha kwa madai yaliyowasilishwa, taarifa kutoka ofisi ya rais ilisema. Ameteua kamati ya watu watano kuchunguza madai hayo.