Accueil / Archives
Archives

Cette rubrique présente les archives avec leurs dates de publication originales. L’article est affiché dans sa langue d’origine.

Rais Ruto ataka uchunguzi wa kina kufanyika kuhusu mauaji ya mbunge Nairobi

Polisi nchini Kenya wanasema mauaji ya kiongozi huyo 'yalipangwa na yalikuwa mahsusi' Rais William Ruto ametoa wito kwa polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji ya mbunge Charles Ong’ondo Were aliyeuawa Jumatano usiku na waliohusika kuwajibishwa kisheria. Alitoa salamu zake za rambirambi ku...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Mis à jour 13/08/2026 05:26:19
Rais Ruto ataka uchunguzi wa kina kufanyika kuhusu mauaji ya mbunge Nairobi
En bref

Polisi nchini Kenya wanasema mauaji ya kiongozi huyo 'yalipangwa na yalikuwa mahsusi' Rais William Ruto ametoa wito kwa polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji ya mbunge Charles Ong’ondo Were aliyeuawa Jumatano usiku na waliohusika kuwajibishwa kisheria. Alitoa salamu zake za rambirambi ku...

Polisi nchini Kenya wanasema mauaji ya kiongozi huyo 'yalipangwa na yalikuwa mahsusi' Rais William Ruto ametoa wito kwa polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji ya mbunge Charles Ong’ondo Were aliyeuawa Jumatano usiku na waliohusika kuwajibishwa kisheria. Alitoa salamu zake za rambirambi kupitia mtandao wa X akisema ‘‘Mungu aifariji familia na awape nguvu watu wa Kasipul kutokana na kifo cha Mheshimiwa Charles Ong’ondo Were’’, alisema Ruto. ‘‘Tunatoa wito kwa polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo. Na wale waliohusika kuwajibishwa,’’ aliongeza. Polisi nchini Kenya wanasema mbunge huyo aliuawa kwa kupigwa risasi na mtu asiyejulikana ambaye alikuwa kwenye pikipiki katika mji mkuu, Nairobi Jumatano usiku. Polisi waliongeza kuwa mauaji hayo yanaonekana kupangwa na yenye lengo mahsusi. Charles Were, anayewakilisha eneo bunge la Kasipul lililoko magharibi mwa Kenya, alipigwa risasi na kuuawa saa moja na nusu usiku wakati gari lake liliposimama kusubiri taa kwenye barabara ya Ngong, polisi walisema kwenye taarifa waliyoitoa siku ya Jumatano.