Rais Paul Kagame pia alieleza shukrani kwa "jukumu muhimu la Qatar katika juhudi za upatanishi katika migogoro mbalimbali, ikiwemo katika eneo la Maziwa Makuu." Rais wa Rwanda, Paul Kagame, alikutana na Emir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, siku ya Ijumaa ambapo alionyesha mshikamano na taifa hilo la Ghuba kufuatia shambulio la Israel dhidi ya Doha. Kagame pia alitoa rambirambi zake kwa vifo vilivyotokea wakati wa shambulio hilo, kulingana na taarifa kutoka ofisi yake. “Mazungumzo yao yalisisitiza umuhimu wa uwajibikaji na kutafuta suluhisho la haki kwa mzozo unaoendelea katika eneo hilo,” taarifa hiyo ilisema. Rwanda ilikuwa miongoni mwa mataifa ya Afrika yaliyolaani shambulio la Israel siku ya Jumanne lililolenga wapatanishi wa Hamas huko Doha. Kigali ilikemea "unafiki na kutojali" kwa jumuiya ya kimataifa mbele ya mvutano unaozidi kuongezeka katika Mashariki ya Kati.
News archive
This section shows archived news with its original publication dates. The article is displayed in its original language.
Rais Kagame, akutana na kiongozi wa Qatar, kuonyesha mshikamano baada ya shambulio la Israel
Rais Paul Kagame pia alieleza shukrani kwa "jukumu muhimu la Qatar katika juhudi za upatanishi katika migogoro mbalimbali, ikiwemo katika eneo la Maziwa Makuu." Rais wa Rwanda, Paul Kagame, alikutana na Emir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, siku ya Ijumaa ambapo alionyesha mshikamano na...
At a glance