Home / News archive
News archive

This section shows archived news with its original publication dates. The article is displayed in its original language.

Rais Cyril Ramaphosa na Donald Trump ‘watofautiana’ kuhusu wakulima wazungu

Ni kitu cha ajabu. Sijawahi kuona kitu kama hicho,” alisema Rais wa Marekani Donaldo Trump akizungumzia madai ya mateso dhidi ya wakulima wazungu nchini Afrika Kusini. Rais wa Marekani Donald Trump ametofautiana na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kuhusiana na madai ya mateso na mauaji ya wa...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Updated 13/08/2026, 05:26:19
Rais Cyril Ramaphosa na Donald Trump ‘watofautiana’ kuhusu wakulima wazungu
At a glance

Ni kitu cha ajabu. Sijawahi kuona kitu kama hicho,” alisema Rais wa Marekani Donaldo Trump akizungumzia madai ya mateso dhidi ya wakulima wazungu nchini Afrika Kusini. Rais wa Marekani Donald Trump ametofautiana na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kuhusiana na madai ya mateso na mauaji ya wa...

Ni kitu cha ajabu. Sijawahi kuona kitu kama hicho,” alisema Rais wa Marekani Donaldo Trump akizungumzia madai ya mateso dhidi ya wakulima wazungu nchini Afrika Kusini. Rais wa Marekani Donald Trump ametofautiana na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kuhusiana na madai ya mateso na mauaji ya wakulima wazungu nchini Afrika Kusini. Katika kikao chao kilichofanyika ndani ya ofisi ya Trump ya ‘Oval Office’, siku ya Jumatano, Trump alidai kuwa anao ushahidi wa matukio yenye kuwalenga wakulima wazungu nchini Afrika Kusini, ikiwemo uwepo wa makaburi ya wakulima hao. "Hili ni jambo baya sana. Kuna makaburi zaidi ya 1,000 ya wazungu pale," alisema Rais Trump wakati akicheza video fupi ndani ya ofisi yake. "Mheshimiwa Rais, walikueleza ni wapi hayo yalitokea?" alihoji Rais Ramaphosa kwa utulivu. "Hapana,” alijibu Trump, huku Ramaphosa akisisitiza kuwa alitaka kufahamu zaidi kuhusu video hiyo. "Nilimanisha ni Afrika Kusini,” alisema Trump. Wakati wa kikao hicho, Rais Trump anadaiwa kumwambia Ramaphosa kuwa serikali yake iliruhusu “kuchukuliwa kwa mashamba ya wakulima wazungu, kutoka jamii ya Kiafrikana kuchukuliwa na kisha kuwauwa wakulima hao”. Hata hivyo, Ramaphosa alikana madai hayo, akisisitiza kuwa Afrika Kusini inaendelea na jitihada za kupambana na uhalifu. "Wanaouwawa sio wazungu. Wengi wao ni watu weusi,” alisema Ramaphosa.