Mwanzo / Kumbukumbu za habari
Kumbukumbu za habari

Sehemu hii inaonyesha habari za kumbukumbu pamoja na tarehe zake za awali za kuchapishwa. Habari imeonyeshwa katika lugha yake ya asili.

Raia wa Japan afungwa jela mwaka mmoja kwa kuua sungura

Hotta alikamatwa mwezi Januari baada ya kupatikana akimpiga teke sungura katika kisiwa cha Okuno. Mahakama nchini Japan, imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela raia wa nchi hiyo kwa kosa la kujeruhi na kuua sungura saba. Riku Hotta, alihukumiwa siku ya Jumatatu kufuatia kosa hilo alilolitenda ka...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Imesasishwa 13/8/2026, 05:26:19
Raia wa Japan afungwa jela mwaka mmoja kwa kuua sungura
Kwa muhtasari

Hotta alikamatwa mwezi Januari baada ya kupatikana akimpiga teke sungura katika kisiwa cha Okuno. Mahakama nchini Japan, imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela raia wa nchi hiyo kwa kosa la kujeruhi na kuua sungura saba. Riku Hotta, alihukumiwa siku ya Jumatatu kufuatia kosa hilo alilolitenda ka...

Hotta alikamatwa mwezi Januari baada ya kupatikana akimpiga teke sungura katika kisiwa cha Okuno. Mahakama nchini Japan, imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela raia wa nchi hiyo kwa kosa la kujeruhi na kuua sungura saba. Riku Hotta, alihukumiwa siku ya Jumatatu kufuatia kosa hilo alilolitenda katika kisiwa cha Okuno kilichopo Hiroshima, eneo ambalo linajulikana pia kama ‘Kisiwa cha Sungura’. Mahakama ya Wilaya ya Hiroshima ilimkuta Hotta na hatia ya kuua sungura wapatao saba, huku Jaji Wataru Shimazaki akikiita kuwa ni kitendo “kiovu”. Hotta alikamatwa mwezi Januari baada ya kupatikana akimpiga sungura teke katika kisiwa hicho. Mnyama huyo aliripotiwa kufa kutokana na majeraha aliyoyapata. Kufuatia tukio hilo, Wizara ya Mazingira nchini Japan imepanga kufunga kamera za siri ndani ya kisiwa hicho ili kubaini matukio mengine kama hayo.