Mamlaka ya Mashtaka ya Kitaifa (NPA) imepongeza hukumu hiyo kama hatua muhimu katika vita dhidi ya biashara haramu ya binadamu nchini Afrika Kusini. Mahakama ya Afrika Kusini imewahukumu kifungo cha miaka 20 gerezani raia saba wa China kwa kosa la utekaji nyara na kazi za kulazimishwa, kulingana na taarifa kutoka kwa shirika la habari la serikali. Walithibitishwa kuwa na hatia mwanzoni mwa mwaka huu kwa utekaji nyara na kazi za kulazimishwa zinazohusisha raia 91 wa Malawi. Hukumu hii inatokea baada ya kukamatwa kwao miaka sita iliyopita wakati polisi walipotekeleza operesheni ya kukamata watu katika kiwanda kimoja mjini Johannesburg, mji wa kibiashara, ambapo wahamiaji haramu wakiwemo watoto waliopatwa wakifanya kazi chini ya hali mbaya sana, ripoti za SABC zinasema.
Sehemu hii inaonyesha habari za kumbukumbu pamoja na tarehe zake za awali za kuchapishwa. Habari imeonyeshwa katika lugha yake ya asili.
Raia wa China wahukumiwa miaka 20 jela kwa kosa la utekaji nyara Afrika Kusini
Mamlaka ya Mashtaka ya Kitaifa (NPA) imepongeza hukumu hiyo kama hatua muhimu katika vita dhidi ya biashara haramu ya binadamu nchini Afrika Kusini. Mahakama ya Afrika Kusini imewahukumu kifungo cha miaka 20 gerezani raia saba wa China kwa kosa la utekaji nyara na kazi za kulazimishwa, kulingana...