Gida / Taskar labarai
Taskar labarai

Wannan sashe yana nuna tsoffin labarai da ranakun da aka wallafa su. An nuna labarin a harshensa na asali.

Motsepe: AFCON 2027 itafanyika Afrika Mashariki na si kwingineko

Michuano hiyo inaandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda. Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe anaamini kuwa michuano ya AFCON 2027 itafanyika Afrika Mashariki, kama ilivyopangwa na wala haitohairishwa hadi mwaka 2028. Akizungumza Februari 13, jijini Dar es Salaam, Mot...

NewstimeTR Haber Merkezi · · An sabunta 2026-08-13, 05:26:18
Motsepe: AFCON 2027 itafanyika Afrika Mashariki na si kwingineko
A taƙaice

Michuano hiyo inaandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda. Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe anaamini kuwa michuano ya AFCON 2027 itafanyika Afrika Mashariki, kama ilivyopangwa na wala haitohairishwa hadi mwaka 2028. Akizungumza Februari 13, jijini Dar es Salaam, Mot...

Michuano hiyo inaandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda. Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe anaamini kuwa michuano ya AFCON 2027 itafanyika Afrika Mashariki, kama ilivyopangwa na wala haitohairishwa hadi mwaka 2028. Akizungumza Februari 13, jijini Dar es Salaam, Motsepe alisisitiza kuwa kuwa ana imani na matayarisho yaliyofanywa na mashirikisho ya soka ya Tanzania, Kenya na Uganda kama wenyeji wa michuano hiyo mikubwa barani Afrika. “Nina imani kuwa michuano ya AFCON itafanyika hapa, kwahiyo sitaki kusikia swali la michuano ya AFCON kuhamishiwa sehemu nyingine,” alisema Motsepe. “Tunafahamu kuna changamoto za hapa na pale, lakini ni muhimu kuendelea kuaminiana na kuungana mkono kama Waafrika, kwani inawezekana.”