Accueil / Archives
Archives

Cette rubrique présente les archives avec leurs dates de publication originales. L’article est affiché dans sa langue d’origine.

Mlima Kilimanjaro wang'ara kati ya maeneo ya kuvutia kwa picha ulimwenguni

Jumla ya wapandaji 50,000 hukwea mlima huo kila mwaka, huku ukivutia watumiaji wa mitandao zaidi ya milioni 5.5 kila mwaka. Mlima Kilimanjaro umeshika nafasi ya pili katika kipengele cha maeneo yenye kuvutia zaidi kwa picha duniani, kulingana na utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na taasisi ya H...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Mis à jour 13/08/2026 05:26:17
Mlima Kilimanjaro wang'ara kati ya maeneo ya kuvutia kwa picha ulimwenguni
En bref

Jumla ya wapandaji 50,000 hukwea mlima huo kila mwaka, huku ukivutia watumiaji wa mitandao zaidi ya milioni 5.5 kila mwaka. Mlima Kilimanjaro umeshika nafasi ya pili katika kipengele cha maeneo yenye kuvutia zaidi kwa picha duniani, kulingana na utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na taasisi ya H...

Jumla ya wapandaji 50,000 hukwea mlima huo kila mwaka, huku ukivutia watumiaji wa mitandao zaidi ya milioni 5.5 kila mwaka. Mlima Kilimanjaro umeshika nafasi ya pili katika kipengele cha maeneo yenye kuvutia zaidi kwa picha duniani, kulingana na utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na taasisi ya Heepsy. Mlima huo, ambao unapatikana nchini Tanzania, umeshika nafasi ya pili nyuma ya jengo la Burj Khalifa la Dubai na pia kuushinda mnara wa Eiffel unaopatikana nchini Ufaransa. Jumla ya wapandaji 50,000 hukwea mlima huo kila mwaka, huku ukivutia watumiaji wa mitandao zaidi ya milioni 5.5 kila mwaka. Nafasi ya nne imechukuliwa na mnara wa saa wa jijini London, maarufu kama ‘Big Ben’, wakati visiwa vya Galápagos vya nchini Ecuador vikiwa katika nafasi ya tano.