Inicio / Archivo de noticias
Archivo de noticias

Esta sección muestra noticias archivadas con sus fechas de publicación originales. El artículo se muestra en su idioma original.

Mkuu wa Majeshi wa Uganda aiomba radhi Marekani

Mkuu wa Majeshi nchini Uganda, Muhoozi Kainerugaba aiomba radhi Marekani kufuatia 'tweets' zake za awali. Mkuu wa Majeshi wa Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameiomba radhi serikali ya Marekani, baada yeye mwenyewe, kuweka jumbe tata, kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter), ambazo ba...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Actualizado 13/8/2026, 5:26:17
Mkuu wa Majeshi wa Uganda aiomba radhi Marekani
De un vistazo

Mkuu wa Majeshi nchini Uganda, Muhoozi Kainerugaba aiomba radhi Marekani kufuatia 'tweets' zake za awali. Mkuu wa Majeshi wa Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameiomba radhi serikali ya Marekani, baada yeye mwenyewe, kuweka jumbe tata, kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter), ambazo ba...

Mkuu wa Majeshi nchini Uganda, Muhoozi Kainerugaba aiomba radhi Marekani kufuatia 'tweets' zake za awali. Mkuu wa Majeshi wa Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameiomba radhi serikali ya Marekani, baada yeye mwenyewe, kuweka jumbe tata, kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter), ambazo baadaye alizifuta. Katika jumbe hizo, Muhoozi alidai kuwa Ubalozi wa Marekani wa jijini Kampala, ulikuwa unahusishwa na siasa za upinzani nchini humo, na hata kutangaza kusitishwa kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Uganda na Marekani. Kauli hizo zilizua taharuki na wasiwasi wa kidiplomasia. Jenerali Muhoozi ambaye pia ni mwana wa Rais wa Uganda alieleza kuwa amezungumza na Balozi wa Marekani nchini Uganda na kuthibitisha kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili bado uko sawa.