Mwanzo / Kumbukumbu za habari
Kumbukumbu za habari

Sehemu hii inaonyesha habari za kumbukumbu pamoja na tarehe zake za awali za kuchapishwa. Habari imeonyeshwa katika lugha yake ya asili.

Mashirika ya ndege ya Qatar na Kenya kushirikiana

Qatar Airways na Kenya Airways wametia saini makubaliano yatakayowezesha abiria kusafiri katika maeneo mbalimbali duniani. Mashirika ya ndege ya Qatar Airways na Kenya Airways yametangaza kuzindua mfumo wa ushirikiano utakawaofikisha wateja wao katika maeneo 19, huku maeneo mengine yakitarajiwa k...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Imesasishwa 13/8/2026, 05:26:17
Mashirika ya ndege ya Qatar na Kenya kushirikiana
Kwa muhtasari

Qatar Airways na Kenya Airways wametia saini makubaliano yatakayowezesha abiria kusafiri katika maeneo mbalimbali duniani. Mashirika ya ndege ya Qatar Airways na Kenya Airways yametangaza kuzindua mfumo wa ushirikiano utakawaofikisha wateja wao katika maeneo 19, huku maeneo mengine yakitarajiwa k...

Qatar Airways na Kenya Airways wametia saini makubaliano yatakayowezesha abiria kusafiri katika maeneo mbalimbali duniani. Mashirika ya ndege ya Qatar Airways na Kenya Airways yametangaza kuzindua mfumo wa ushirikiano utakawaofikisha wateja wao katika maeneo 19, huku maeneo mengine yakitarajiwa kuongezwa hivi karibuni. Abiria wa Kenya Airways sasa wanaweza kuunganisha safari zao katika miji kumi kati ya Nairobi na Doha, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad. Vilevile, wateja wa shirika la ndege la Qatar Airways wanaweza kufika katika maeneo nane kwa kutumia mtandao wa Kenya Airways, kutokana na safari tatu za ndege za kila siku kati ya Doha na Nairobi . Wateja wataweza kusafiri kwa kutumia mfumo huu kuanzia tarehe 26 Oktoba 2025. Uuzaji wa tiketi kwa ajili ya safari hizo za ndege umeanza Jumanne 21 Oktoba.