Ana Sayfa / Haber arşivi
Haber arşivi

Bu bölüm arşiv haberlerini özgün tarihleriyle gösterir. Haber metni özgün dilinde gösterilmektedir.

Marekani yatoa tahadhari kwa raia wake Tanzania

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, umetoa tahadhari kwa raia wake walioko nchini Tanzania kuwa makini kufuatia maandamano dhidi ya serikai yaliyopangwa kufanyika tarehe 9 Disemba. Hata hivyo ubalozi huo kupitia mtandao wa X, umeongeza kwamba licha ya maandamano hayo kupangwa kufanyika tarehe 9...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Güncellendi 13.08.2026 05:26:17
Marekani yatoa tahadhari kwa raia wake Tanzania
Bu haberde ne var?

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, umetoa tahadhari kwa raia wake walioko nchini Tanzania kuwa makini kufuatia maandamano dhidi ya serikai yaliyopangwa kufanyika tarehe 9 Disemba. Hata hivyo ubalozi huo kupitia mtandao wa X, umeongeza kwamba licha ya maandamano hayo kupangwa kufanyika tarehe 9...

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, umetoa tahadhari kwa raia wake walioko nchini Tanzania kuwa makini kufuatia maandamano dhidi ya serikai yaliyopangwa kufanyika tarehe 9 Disemba. Hata hivyo ubalozi huo kupitia mtandao wa X, umeongeza kwamba licha ya maandamano hayo kupangwa kufanyika tarehe 9 Disemba, huenda yakaanza mapema tarehe 5. Aidha, ubalozi huo umesema yoyote anayepanga kusafiri nchini Tanzania, ajipange kwa usumbufu wa usafiri, ikiwemo safari za ndege njia za barabarani na baharini, na kuzimwa kwa mtandao wa intaneti pamoja na amri ya kutotoka nje. Taarifa hiyo pia ilisema, kufuatia vurugu zilizoshuhudiwa nchini humo, vyombo vya usalama vimeanza kuwalenga raia wa kigeni wakisaka vifaa vya elektroniki vinavyosambaza ushahidi wa ghasia zilizotokea. Polisi imetahadharisha ya kwamba kusambazwa kwa picha au video zitakazosababisha taharuki nchini ni uhalifu chini ya sheria ya Tanzania.