Mwanzo / Kumbukumbu za habari
Kumbukumbu za habari

Sehemu hii inaonyesha habari za kumbukumbu pamoja na tarehe zake za awali za kuchapishwa. Habari imeonyeshwa katika lugha yake ya asili.

Mapigano mapya yazuka siku chache kabla ya Tshisekedi na Kagame kutiliana saini mkataba wa amani

Katika taarifa yake kuhusu mapigano hayo, Jeshi la Ulinzi la nchini DRC (FARDC), limeituhumu Rwanda kwa kushirikiana na kikundi cha waasi wa M23 kwa kuratibu mfululizo wa mashambulizi katika maeneo ya Kaziba, Katogota na Lubarika. Mapigano mapya kati ya waasi wa M23 na jeshi la Jamhuri ya Kidemok...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Imesasishwa 13/8/2026, 05:26:17
Mapigano mapya yazuka siku chache kabla ya Tshisekedi na Kagame kutiliana saini mkataba wa amani
Kwa muhtasari

Katika taarifa yake kuhusu mapigano hayo, Jeshi la Ulinzi la nchini DRC (FARDC), limeituhumu Rwanda kwa kushirikiana na kikundi cha waasi wa M23 kwa kuratibu mfululizo wa mashambulizi katika maeneo ya Kaziba, Katogota na Lubarika. Mapigano mapya kati ya waasi wa M23 na jeshi la Jamhuri ya Kidemok...

Katika taarifa yake kuhusu mapigano hayo, Jeshi la Ulinzi la nchini DRC (FARDC), limeituhumu Rwanda kwa kushirikiana na kikundi cha waasi wa M23 kwa kuratibu mfululizo wa mashambulizi katika maeneo ya Kaziba, Katogota na Lubarika. Mapigano mapya kati ya waasi wa M23 na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yalizuka siku ya Jumanne, katika maeneo tofauti ya Mashariki mwa DRC. Mapigano hayo yalizuka asubuhi ya Jumanne katika maeneo ya Walungu na Uvira, huko kusini mwa jimbo la Kivu, na kutatiza masomo na biashara. Baadhi ya wakulima waliokuwa mashambani mwao, waliripotiwa kutafuta maeneo ya usalama, baada ya mapigano hayo kuzidi kuongezeka kwenye eneo la Kamanyola. Katika taarifa yake kuhusu mapigano hayo, Jeshi la Ulinzi la nchini DRC (FARDC), limeituhumu Rwanda kwa kushirikiana na kikundi cha waasi wa M23 kwa kuratibu mfululizo wa mashambulizi katika maeneo ya Kaziba, Katogota na Lubarika. Hivi karibuni, serikali ya DRC na kikundi cha M23 zilitiliana saini mkataba wa amani jijini Doha, ukisimamiwa na Qatar.