Mwanzo / Kumbukumbu za habari
Kumbukumbu za habari

Sehemu hii inaonyesha habari za kumbukumbu pamoja na tarehe zake za awali za kuchapishwa. Habari imeonyeshwa katika lugha yake ya asili.

Malawi yapiga marufuku usafirishaji wa mazao kuimarisha usalama wa chakula

Hatua hiyo inafuatia nchi hiyo kukumbukwa na vimbunga vilivyoathiri uzalishaji wa chakula. Serikali ya Malawi imepiga marufuku usafirishaji nje wa mazao kwa lengo la kukuza usalama wa chakula nchini humo. Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii wa nchini Malawi Charity Musonzo alisema kuwa mpango h...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Imesasishwa 13/8/2026, 05:26:17
Malawi yapiga marufuku usafirishaji wa mazao kuimarisha usalama wa chakula
Kwa muhtasari

Hatua hiyo inafuatia nchi hiyo kukumbukwa na vimbunga vilivyoathiri uzalishaji wa chakula. Serikali ya Malawi imepiga marufuku usafirishaji nje wa mazao kwa lengo la kukuza usalama wa chakula nchini humo. Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii wa nchini Malawi Charity Musonzo alisema kuwa mpango h...

Hatua hiyo inafuatia nchi hiyo kukumbukwa na vimbunga vilivyoathiri uzalishaji wa chakula. Serikali ya Malawi imepiga marufuku usafirishaji nje wa mazao kwa lengo la kukuza usalama wa chakula nchini humo. Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii wa nchini Malawi Charity Musonzo alisema kuwa mpango huwa unalenga la kuhuisha usambazaji wa chakula, kudhibiti bei za mazao ya chakula na kulinda uhai wa wananchi wa Malawi wenye kutegema mahindi kama zao lao la chakula. “Zao la mahindi lipo chini Sheria ya Udhibiti wa mazao, hivyo ni makosa kusafirisha bila ruhusa maalumu,” alisema Musonzo. Malawi inakabaliana na uhaba mkubwa wa chakula ambao umeathiri takribani watu milioni 4. Wakati ufunguzi wa mwaka wa bajeti kwa mwaka 2025, Rais Arthur Peter Mutharika aliielezea hali hiyo kama janga la kitaifa akiitaka jumuiya ya kimataifa kutoa msaada.