Mwanzo / Kumbukumbu za habari
Kumbukumbu za habari

Sehemu hii inaonyesha habari za kumbukumbu pamoja na tarehe zake za awali za kuchapishwa. Habari imeonyeshwa katika lugha yake ya asili.

Kuridhia kwa serikali ya Eswatini kupokea waliotimuliwa Marekani kwapinga mahakamani

Wanaharakati wa Eswatini wameiomba mahakama kuu kuamua kuwa kinyume cha katiba hatua ya nchi hiyo kukubali kuwapokea raia watano wa kigeni ambao walifukuzwa Marekani. Wanaharakati wa Eswatini wameitaka mahakama kuu kuamia kuwa ni kinyume cha katiba kwa nchi yao kukubali kuwapokea raia watano wa n...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Imesasishwa 13/8/2026, 05:26:14
Kuridhia kwa serikali ya Eswatini kupokea waliotimuliwa Marekani kwapinga mahakamani
Kwa muhtasari

Wanaharakati wa Eswatini wameiomba mahakama kuu kuamua kuwa kinyume cha katiba hatua ya nchi hiyo kukubali kuwapokea raia watano wa kigeni ambao walifukuzwa Marekani. Wanaharakati wa Eswatini wameitaka mahakama kuu kuamia kuwa ni kinyume cha katiba kwa nchi yao kukubali kuwapokea raia watano wa n...

Wanaharakati wa Eswatini wameiomba mahakama kuu kuamua kuwa kinyume cha katiba hatua ya nchi hiyo kukubali kuwapokea raia watano wa kigeni ambao walifukuzwa Marekani. Wanaharakati wa Eswatini wameitaka mahakama kuu kuamia kuwa ni kinyume cha katiba kwa nchi yao kukubali kuwapokea raia watano wa nje ambao walitimuliwa kutoka Marekani baada ya kuwepo gerezani kwa hatia ikiwemo mauaji. Wanaume hao kutoka Vietnam, Laos, Yemen, Cuba na Jamaica walisafirishwa hadi katika taifa hilo la Kusini mwa Afrika kwa ndege ya kijeshi ya Marekani mwezi Julai ikiwa ni sehemu ya mpango wa Marekani wa kuwapeleka wahamiaji katika mataifa ya tatu. Katika shauri la dharura kwenye mahakama kuu ya Eswatini, mashirika matatu ya kisheria na ya kiraia yanasema makubaliano ni kinyume cha katiba kwa sababu hayakuwa yamewekwa wazi na hakukuwepo na mashauriano ya umma au bunge. Walitaka serikali ya Eswatini kuweka wazi makubaliano kamili na Marekani.