Mwanzo / Kumbukumbu za habari
Kumbukumbu za habari

Sehemu hii inaonyesha habari za kumbukumbu pamoja na tarehe zake za awali za kuchapishwa. Habari imeonyeshwa katika lugha yake ya asili.

Kiongozi wa upinzani Uganda, Bobi Wine kuwania urais

Katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2021, Wine alikuwa wa pili, lakini alikataa matokeo, na kudai kulikuwa na wizi wa kura. Tuhuma ambazo serikali na Tume ya Uchaguzi ilizikana. Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na msanii Bobi Wine, amesema Ijumaa kuwa ana mpango wa kugombea urais wa nchi hiyo kwa...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Imesasishwa 13/8/2026, 05:26:14
Kiongozi wa upinzani Uganda, Bobi Wine kuwania urais
Kwa muhtasari

Katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2021, Wine alikuwa wa pili, lakini alikataa matokeo, na kudai kulikuwa na wizi wa kura. Tuhuma ambazo serikali na Tume ya Uchaguzi ilizikana. Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na msanii Bobi Wine, amesema Ijumaa kuwa ana mpango wa kugombea urais wa nchi hiyo kwa...

Katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2021, Wine alikuwa wa pili, lakini alikataa matokeo, na kudai kulikuwa na wizi wa kura. Tuhuma ambazo serikali na Tume ya Uchaguzi ilizikana. Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na msanii Bobi Wine, amesema Ijumaa kuwa ana mpango wa kugombea urais wa nchi hiyo kwa mara ya pili huku akizilaumu nchi za magharibi kwa kufumbia macho “ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu” anaodai unafanyika nchini mwake. Wine, wenye umri wa miaka 43, ambae jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, kwa mara nyengine ataingia katika kinyang’anyiro hicho na mpinzani wake, ambae ni rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Yoweri Museveni, mwenye miaka 80. Wengi wanatarajia Rais Museveni atasimama tena. “Ndio, nimeelezea kupatikana kwangu kwa niaba ya timu yangu,” amenukuliwa Wine katika mahojiano na Reuters pindi alipoulizwa iwapo ana nia ya kusimama tena katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, ambao unatarajiwa kufanyika Januari, 2026. Kushiriki katika uchaguzi, amesema Wine, pia itakuwa ni “fursa ya kupambana na kuuanika uongozi na kuunganisha watu wa Uganda kusimama ili kujipatia huru wao.” Katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2021, Wine alikuwa wa pili, lakini alikataa matokeo, na kudai kulikuwa na wizi wa kura. Tuhuma ambazo serikali ilizikana.