Início / Arquivo de notícias
Arquivo de notícias

Esta secção apresenta notícias arquivadas com as datas de publicação originais. O artigo é apresentado no idioma original.

Kenya kuanzisha balozi zake mpya Vatican City, Denmark na Vietnam

Kulingana na baraza hilo, uwepo wa ofisi ya ubalozi nchini Vatican, ni wa faida kwa Kenya, kutokana na fursa za maendeleo ya miradi ya kijamii kama vile elimu na dini. Baraza la Mawaziri la Kenya lililoketi Jumanne jioni, limeidhinisha uanzishwaji wa ofisi mpya za ubalozi Vatican City, Denmark na...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Atualizado 13/08/2026, 05:26:13
Kenya kuanzisha balozi zake mpya Vatican City, Denmark na Vietnam
Em resumo

Kulingana na baraza hilo, uwepo wa ofisi ya ubalozi nchini Vatican, ni wa faida kwa Kenya, kutokana na fursa za maendeleo ya miradi ya kijamii kama vile elimu na dini. Baraza la Mawaziri la Kenya lililoketi Jumanne jioni, limeidhinisha uanzishwaji wa ofisi mpya za ubalozi Vatican City, Denmark na...

Kulingana na baraza hilo, uwepo wa ofisi ya ubalozi nchini Vatican, ni wa faida kwa Kenya, kutokana na fursa za maendeleo ya miradi ya kijamii kama vile elimu na dini. Baraza la Mawaziri la Kenya lililoketi Jumanne jioni, limeidhinisha uanzishwaji wa ofisi mpya za ubalozi Vatican City, Denmark na Vietnam. Katika kikao chake kilichofanyika Ikulu ya Nairobi, baraza hilo limesema kuwa hatua ya kuanzisha balozi ndani ya Makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, itakuza mahusiano kati ya mataifa hayo matatu. “Uanzishwaji wa ubalozi wetu huko Vatican utaimarisha uhusiano wetu na taasisi za maendeleo za Kikatoliki ambazo zinaendesha jumla ya shule 7,700 na vituo vya afya 500 nchi nzima,” ilisomeka sehemu ya taarifa ya baraza hilo. Kulingana na baraza hilo, uwepo wa ofisi ya ubalozi nchini Vatican, ni wa faida kwa Kenya, kutokana na fursa za maendeleo ya miradi ya kijamii kama vile elimu na dini.