Mwanzo / Kumbukumbu za habari
Kumbukumbu za habari

Sehemu hii inaonyesha habari za kumbukumbu pamoja na tarehe zake za awali za kuchapishwa. Habari imeonyeshwa katika lugha yake ya asili.

Ivory Coast yamrejesha kikosini Wilfred Zaha kwa ajili ya fainali za AFCON

Zaha, mwenye umri wa miaka 33, ambaye kwa sasa anachezea timu ya Charlotte, inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Marekani, alikuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 26 ambacho kitakabaliana Msumbiji, Cameroon na Gabon kwenye Kundi F. Mabingwa watetezi wa Kombe la AFCON, Ivory Coast imemrudisha kikosini w...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Imesasishwa 13/8/2026, 05:26:12
Ivory Coast yamrejesha kikosini Wilfred Zaha kwa ajili ya fainali za AFCON
Kwa muhtasari

Zaha, mwenye umri wa miaka 33, ambaye kwa sasa anachezea timu ya Charlotte, inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Marekani, alikuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 26 ambacho kitakabaliana Msumbiji, Cameroon na Gabon kwenye Kundi F. Mabingwa watetezi wa Kombe la AFCON, Ivory Coast imemrudisha kikosini w...

Zaha, mwenye umri wa miaka 33, ambaye kwa sasa anachezea timu ya Charlotte, inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Marekani, alikuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 26 ambacho kitakabaliana Msumbiji, Cameroon na Gabon kwenye Kundi F. Mabingwa watetezi wa Kombe la AFCON, Ivory Coast imemrudisha kikosini winga wa zamani wa Crystal Palace, Wilfried Zaha kwa ajili ya michuano ya AFCON 2025 itakayofanyika nchini Morocco. Zaha, mwenye umri wa miaka 33, ambaye kwa sasa anachezea timu ya Charlotte, inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Marekani, alikuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 26 ambacho kitakabaliana Msumbiji, Cameroon na Gabon kwenye Kundi F. Zaha aliondolewa kwenye kikosi cha Tembo hao mwaka jana, baada ya timu ya taifa ya Ivory Coast ilipopenya kwenye hatua ya mtoano, kabla haijafunga Nigeria kwa mabao 2-1 kwenye fainali iliyofanyika jijini Abidjan. "Tunahitaji wachezaji wazoefu. Zaha ana uwezo wa kuwakabili mabeki," alisema kocha Emerse Fae wakati akitangaza kikosi hicho kwenye televisheni ya nchi hiyo. Zaha, ambaye alishiriki michezo minne tu akiwa na Manchester United akiwa Old Trafford kwa misimu miwili kabla ya kurejea Palace, alishiriki michezo miwili ya kimataifa akiwa na jezi ya England, kabla ya kuhamia kuichezea Ivory Coast.