Home / News archive
News archive

This section shows archived news with its original publication dates. The article is displayed in its original language.

Ethiopia yakana kufadhiliwa na Marekani ujenzi wa bwawa la umeme

Kulingana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, bwawa hilo lilijengwa kwa kutumia fedha za ndani za nchi hiyo. Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema kuwa nchi yake haikupokea “senti” yoyote kutoka nchi yoyote ya nje, ili kufanikisha ujenzi wa bwawa la kufua umeme, maarufu kama Grand Ethiopian Renaissa...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Updated 13/08/2026, 05:26:10
Ethiopia yakana kufadhiliwa na Marekani ujenzi wa bwawa la umeme
At a glance

Kulingana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, bwawa hilo lilijengwa kwa kutumia fedha za ndani za nchi hiyo. Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema kuwa nchi yake haikupokea “senti” yoyote kutoka nchi yoyote ya nje, ili kufanikisha ujenzi wa bwawa la kufua umeme, maarufu kama Grand Ethiopian Renaissa...

Kulingana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, bwawa hilo lilijengwa kwa kutumia fedha za ndani za nchi hiyo. Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema kuwa nchi yake haikupokea “senti” yoyote kutoka nchi yoyote ya nje, ili kufanikisha ujenzi wa bwawa la kufua umeme, maarufu kama Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD), akipinga madai ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuwa Marekani iliyofadhili mradi huo. Akihutubia bunge la nchi hiyo, Abiy alisema kuwa ujenzi wa bwawa hilo, ulitekelezwa na vyanzo vya ndani vya Ethiopia. Bwawa hilo, ambalo limejengwa kwenye mto Nile karibu na mpaka wa Sudan, ndiyo bwawa kubwa la kufulia umeme kwa sasa barani Afrika. Akizungumza ndani ya Ikulu ya Marekani mwishoni mwa mwezi Januari, Trump alihoji ni kwa nini serikali ya Marekani ilifadhili mradi huo, madai yaliyopingwa na Ethiopia. Abiy aliongeza kuwa, Ethiopia inakamilisha mradi mwingine wa ufuaji umeme katika mto Omo, utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha gigawati 6,460 za umeme kwa mwaka.