Accueil / Archives
Archives

Cette rubrique présente les archives avec leurs dates de publication originales. L’article est affiché dans sa langue d’origine.

Droni za Ukraine zateketeza ghala la mafuta la Urusi

Ukraine imeendelea kuishambulia hifadhi ya mafuta ya Urusi, kama kisasi baada ya Urusi kuuwa maelfu ya Waukraine. Mashambulizi ya droni za Ukraine yametekeza ghala la mafuta la Urusi katika eneo la kusini la Krasnodar, kulingana na taarifa iliyotolewa na maofisa wa Urusi siku ya Jumapili. Ukraine...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Mis à jour 13/08/2026 05:26:10
Droni za Ukraine zateketeza ghala la mafuta la Urusi
En bref

Ukraine imeendelea kuishambulia hifadhi ya mafuta ya Urusi, kama kisasi baada ya Urusi kuuwa maelfu ya Waukraine. Mashambulizi ya droni za Ukraine yametekeza ghala la mafuta la Urusi katika eneo la kusini la Krasnodar, kulingana na taarifa iliyotolewa na maofisa wa Urusi siku ya Jumapili. Ukraine...

Ukraine imeendelea kuishambulia hifadhi ya mafuta ya Urusi, kama kisasi baada ya Urusi kuuwa maelfu ya Waukraine. Mashambulizi ya droni za Ukraine yametekeza ghala la mafuta la Urusi katika eneo la kusini la Krasnodar, kulingana na taarifa iliyotolewa na maofisa wa Urusi siku ya Jumapili. Ukraine imeendelea kuishambulia hifadhi ya mafuta ya Urusi, kama kisasi baada ya Urusi kuuwa maelfu ya Waukraine. Gavana na wa eneo la Krasnodar Veniamin Kondratyev, alisema kuwa shambulizi hilo lilitokea katika hifadhi iliyopo katika kijiji cha Volna. Eneo hilo, ndimo iliko hifadhi ya mafuta, mkaa na ngano ya Urusi. "Hali ni mbaya zaidi katika eneo la Volna ambapo tenki la mafuta na hifadhi zingine zimeharibiwa vibaya," alisema Kondratyev. Kulingana na Kondratyev, watu wawili walijeruhiwa wakati zaidi ya zimamoto 100 wakipambana kuuzima moto huo. Kwa upande wake, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema kuwa, imefanikiwa kutungua droni 88 za Ukraine katika mipaka iliyo kusini mwa nchi hiyo.