Kulingana na takwimu zilizotolewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) hivi karibuni, taifa hilo linashika nafasi ya 61 ulimwenguni, ikiwa ni ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inashika nafasi ya kwanza kwa ubora wa soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Kulingana na orodha ya FIFA iliyotolewa Julai 10, 2025, DRC ni ya 61 kwa ubora, kati ya mataifa 210. Kwa mujibu wa orodha hiyo, Uganda ni ya pili katika ukanda wa Afrika Mashariki, baada ya kupanda hadi nafasi ya 88 duniani huku Tanzania, nayo ikipanda kwa nafasi nne, hadi nafasi ya 103 duniani, na hivyo kuwa ya tatu kwa ubora Afrika Mashariki. Kenya ni ya 109 ulimwenguni, na ya nne kwa ubora Afrika Mashariki, wakati Rwanda ni ya tano, baada ya kushika nafasi 127 duniani. Burundi ni ya sita kwa ubora, ikifuatiwa na Sudan Kusini huku Somalia ikishika mkia, ikiwa katika nafasi ya 200 ulimwenguni. Kwa upande mwingine, mabingwa wa dunia Argentina wameendelea kushikilia nafasi ya kwanza katika orodha hiyo, huku Morocco ikishika nafasi ya kwanza kwa upande wa bara la Afrika, ikifuatiwa kwa karibu na Senegal iliyo katika nafasi ya 18 duniani.
Arquivo de notícias
Esta secção apresenta notícias arquivadas com as datas de publicação originais. O artigo é apresentado no idioma original.
DRC yaendelea kuongoza kwa ubora wa soka Afrika Mashariki
Kulingana na takwimu zilizotolewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) hivi karibuni, taifa hilo linashika nafasi ya 61 ulimwenguni, ikiwa ni ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inashika nafasi ya kwanza kwa ubora wa soka katika ukanda wa Afrika Mas...
Em resumo