Mwanzo / Kumbukumbu za habari
Kumbukumbu za habari

Sehemu hii inaonyesha habari za kumbukumbu pamoja na tarehe zake za awali za kuchapishwa. Habari imeonyeshwa katika lugha yake ya asili.

China yaionya Marekani kuhusu Taiwan

Kwa muda mrefu, China imekuwa ikidai umiliki wa eneo linalojitawala la Taiwan, huku Marekani nayo, ikiliunga mkono eneo la Taiwan kwa kulipa misaada ya silaha. Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ameionya Marekani kuhusu kupanga njama dhidi ya Taiwan. Kulingana Wang Yi, njama hizo za Marekan...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Imesasishwa 13/8/2026, 05:26:09
China yaionya Marekani kuhusu Taiwan
Kwa muhtasari

Kwa muda mrefu, China imekuwa ikidai umiliki wa eneo linalojitawala la Taiwan, huku Marekani nayo, ikiliunga mkono eneo la Taiwan kwa kulipa misaada ya silaha. Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ameionya Marekani kuhusu kupanga njama dhidi ya Taiwan. Kulingana Wang Yi, njama hizo za Marekan...

Kwa muda mrefu, China imekuwa ikidai umiliki wa eneo linalojitawala la Taiwan, huku Marekani nayo, ikiliunga mkono eneo la Taiwan kwa kulipa misaada ya silaha. Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ameionya Marekani kuhusu kupanga njama dhidi ya Taiwan. Kulingana Wang Yi, njama hizo za Marekani, zitasababisha ugomvi mkubwa kati ya nchi hizo mbili. Akizungumza mjini Munich, Ujerumani wakati wa mkutano wa mambo ya usalama, Wang amesema kuwa kitendo hicho, ni sawa na Marekani ‘kuvuka mstari mwekundu’ wa China. "Kwa vyovoyote vile, suala hili litaleta ugomvi mkubwa kati ya Marekani na China,” alisema. Kwa muda mrefu, China inadai kuwa na umiliki na eneo linalojitawala la Taiwan, huku Marekani nayo, ikiliunga mkono eneo la Taiwan kwa kulipa misaada ya silaha.