Home / News archive
News archive

This section shows archived news with its original publication dates. The article is displayed in its original language.

CHAN 2024: Tanzania yavuna alama sita baada ya kuifunga Mauritania

Michuano ya CHAN 2024 inaandaliwa kwa pamoja na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Tanzania imezidi kuchanja mbuga kwenye michuano ya CHAN 2024 baada ya kuifunga Mauritania kwa bao 1-0, katika mchezo wao wa pili wa Kundi B, uliofanyika Agosti 6, 2025 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Updated 13/08/2026, 05:26:09
CHAN 2024: Tanzania yavuna alama sita baada ya kuifunga Mauritania
At a glance

Michuano ya CHAN 2024 inaandaliwa kwa pamoja na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Tanzania imezidi kuchanja mbuga kwenye michuano ya CHAN 2024 baada ya kuifunga Mauritania kwa bao 1-0, katika mchezo wao wa pili wa Kundi B, uliofanyika Agosti 6, 2025 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es...

Michuano ya CHAN 2024 inaandaliwa kwa pamoja na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Tanzania imezidi kuchanja mbuga kwenye michuano ya CHAN 2024 baada ya kuifunga Mauritania kwa bao 1-0, katika mchezo wao wa pili wa Kundi B, uliofanyika Agosti 6, 2025 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Bao pekee la ‘Taifa Stars’ lilifungwa na Shomari Kapombe aka ‘Baba Esther’ katika dakika ya 89 ya mchezo, na kuipa alama nyingine tatu muhimu kwenye michuano hiyo maalumu kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani. Matokeo hayo yanaifanya Mauritania kubakia na alama moja baada ya suluhu yao ya 0-0 na Madagascar, huku Tanzania ikiongoza kundi hilo, ikiwa na alama sita na magoli matatu, baada ya ushindi wao wa awali dhidi ya Burkina Faso.