Ana Sayfa / Haber arşivi
Haber arşivi

Bu bölüm arşiv haberlerini özgün tarihleriyle gösterir. Haber metni özgün dilinde gösterilmektedir.

Bobi Wine: Mimi si mhalifu

Akizungumzia tishio kutoka kwa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo na mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba, Wine alisema:“Mimi si mhalifu bali mgombea Urais na sio hatia kugombea dhidi ya baba yake.” Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, amesema kuwa...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Güncellendi 13.08.2026 05:26:08
Bobi Wine: Mimi si mhalifu
Bu haberde ne var?

Akizungumzia tishio kutoka kwa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo na mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba, Wine alisema:“Mimi si mhalifu bali mgombea Urais na sio hatia kugombea dhidi ya baba yake.” Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, amesema kuwa...

Akizungumzia tishio kutoka kwa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo na mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba, Wine alisema:“Mimi si mhalifu bali mgombea Urais na sio hatia kugombea dhidi ya baba yake.” Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, amesema kuwa yeye si mhalifu, baada ya kukimbilia mafichoni kufuatia matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa wiki iliyopita nchini humo. Wine, mwenye umri wa miaka 43, anadaiwa kukimbilia kusikojukulikana, baada ya makazi yake kuvamiwa. Wine, ambaye aliuita uchaguzi wa Alhamisi iliyopita kama “wizi wa waziwazi”, amesema kuwa ameendelea kuwa mafichoni, akiwa ulinzi na watu wa ‘kawaida sana’. Akizungumzia tishio kutoka kwa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo na mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba, Wine alisema: “Mimi si mhalifu bali mgombea Urais na sio hatia kugombea dhidi ya baba yake.” Siku ya Jumanne, Kainerugaba, alionesha matamanio yake ya kumrithi baba yake, akiweka wazi azma yake ya kuuondoa uhai wa Wine, kupitia ukurasa wa X. "Tumeua magaidi 22 wa NUP toka wiki iliyopita,” aliandika Kainerugaba. "Ninaomba wa 23 awe Kabobi.”