Gida / Taskar labarai
Taskar labarai

Wannan sashe yana nuna tsoffin labarai da ranakun da aka wallafa su. An nuna labarin a harshensa na asali.

Arsenal na Newcastle wapata ushindi kwenye mechi za Ligi ya mabingwa barani Ulaya

Manchester City yaambulia sare ya 2-2 dhidi ya Monaco licha ya mshambuliaji wao Erling Haaland kupambana kusaidia timu Baadhi ya timu zinazocheza katika Ligi Kuu ya England zilikuwa zinafurahia matokeo yao ya Ligi Kuu ya Mabingwa Ulaya huku wengine wakitafakari mbinu watakayorejea nayo kwenye mec...

NewstimeTR Haber Merkezi · · An sabunta 2026-08-13, 05:26:08
Arsenal na Newcastle wapata ushindi kwenye mechi za Ligi ya mabingwa barani Ulaya
A taƙaice

Manchester City yaambulia sare ya 2-2 dhidi ya Monaco licha ya mshambuliaji wao Erling Haaland kupambana kusaidia timu Baadhi ya timu zinazocheza katika Ligi Kuu ya England zilikuwa zinafurahia matokeo yao ya Ligi Kuu ya Mabingwa Ulaya huku wengine wakitafakari mbinu watakayorejea nayo kwenye mec...

Manchester City yaambulia sare ya 2-2 dhidi ya Monaco licha ya mshambuliaji wao Erling Haaland kupambana kusaidia timu Baadhi ya timu zinazocheza katika Ligi Kuu ya England zilikuwa zinafurahia matokeo yao ya Ligi Kuu ya Mabingwa Ulaya huku wengine wakitafakari mbinu watakayorejea nayo kwenye mechi zao zinazofuata. Arsenal sasa imepata ushindi kwenye mechi zake mbili baada ya kuwafunga Olympiacos 2-0. Meneja wa Arsenal Mikel Arteta alipongeza vijana wake kwa ujasiri na kujituma katika kujihakikishia ushindi huo. Manchester City hawakuwa na bahati baada ya wapinzani wao Monaco kupata penati ya dakika za mwisho na kulazimisha sare ya 2-2. Ni mara ya tatu msimu huu kwa wao kupoteza alama dakika za mwisho mwisho. Newcastle ilipata ushindi wake wa kwanza katika Ligi ya mabingwa barani Ulaya, ikiwa ni ushindi wa kwanza ugenini tangu 2003. Waliifunga Union Gilloise ya Ubelgiji 4-0 PSG iliwafunga Barcelona 2-1 huku Dortmund ikiwacharaza Athletic Bilbao magoli 4-1.