Gida / Taskar labarai
Taskar labarai

Wannan sashe yana nuna tsoffin labarai da ranakun da aka wallafa su. An nuna labarin a harshensa na asali.

Afrika Kusini yakataa kumpokeza Balozi baada ya Marekani kuamua kutoshiriki 'rasmi' G20

Afrika Kusini ni nchi ya kwanza ya Afrika kuongoza mkutano wa G20, ikiwa ni urais wa kupokezana kila mwaka tangu mwezi Disemba na inatarajiwa kuwapokeza Marekani. Msemaji wa Rais Cyril Ramaphosa, Vincent Magwenya, anasema Ramaphosa hatompokeza Balozi mdogo wa Marekani mkutano wa G20 baada ya Mare...

NewstimeTR Haber Merkezi · · An sabunta 2026-08-13, 05:26:07
Afrika Kusini yakataa kumpokeza Balozi baada ya Marekani kuamua kutoshiriki 'rasmi' G20
A taƙaice

Afrika Kusini ni nchi ya kwanza ya Afrika kuongoza mkutano wa G20, ikiwa ni urais wa kupokezana kila mwaka tangu mwezi Disemba na inatarajiwa kuwapokeza Marekani. Msemaji wa Rais Cyril Ramaphosa, Vincent Magwenya, anasema Ramaphosa hatompokeza Balozi mdogo wa Marekani mkutano wa G20 baada ya Mare...

Afrika Kusini ni nchi ya kwanza ya Afrika kuongoza mkutano wa G20, ikiwa ni urais wa kupokezana kila mwaka tangu mwezi Disemba na inatarajiwa kuwapokeza Marekani. Msemaji wa Rais Cyril Ramaphosa, Vincent Magwenya, anasema Ramaphosa hatompokeza Balozi mdogo wa Marekani mkutano wa G20 baada ya Marekani kusisitiza kuwa haitohudhuria mkutano huo rasmi jijini Johannes burg. Mapema Ikulu ya White House ilitoa taarifa fupi ikisema balozi wake mdogo mjini Pretoria angehudhuria hafla ya kupokezana kama taratibu tu mwishoni mwa mkutano wa G20 wikiendi. Balozi mdogo ndiyo aliyekuwa amepewa jukumu hilo, akiwa ni cheo cha chini cha balozi au waziri. Kulingana na Makumbusho ya Kitaifa ya Diplomasia Marekani, bado cheo hicho kinatumika kama mkuu wa ujumbe wa Marekani katika maeneo ambayo Marekani hayana uhusiano mzuri wa kidiplomasia na nchi hiyo. "Balozi au mwakilishi wa ubalozi nchini Afrika Kusini anakuwepo pale tu kuthibitisha kuwa Marekani itakuwa mwenyeji wa mkutano wa G20; watapokea jukumu hilo mwishoni mwa hafla yenyewe, hawatokuwepo hapo kushiriki katika mazungumo rasmi," Msemaji wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt aliwaambia waandishi wa habari.