Inicio / Archivo de noticias
Archivo de noticias

Esta sección muestra noticias archivadas con sus fechas de publicación originales. El artículo se muestra en su idioma original.

Afrika Kusini yafuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya kuifunga Rwanda

Afrika Kusini imekuwa taifa la hivi karibuni kutoka Afrika kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 baada ya kuichapa Rwanda mabao 3-0 siku ya Jumanne na kuongoza kundi C. Timu hiyo ya Bafana bafana imefuzu Kombe la Dunia licha ya kuondolewa pointi tatu kwa kumchezesha mchezaji asiyestahili katika mechi...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Actualizado 13/8/2026, 5:26:07
Afrika Kusini yafuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya kuifunga Rwanda
De un vistazo

Afrika Kusini imekuwa taifa la hivi karibuni kutoka Afrika kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 baada ya kuichapa Rwanda mabao 3-0 siku ya Jumanne na kuongoza kundi C. Timu hiyo ya Bafana bafana imefuzu Kombe la Dunia licha ya kuondolewa pointi tatu kwa kumchezesha mchezaji asiyestahili katika mechi...

Afrika Kusini imekuwa taifa la hivi karibuni kutoka Afrika kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 baada ya kuichapa Rwanda mabao 3-0 siku ya Jumanne na kuongoza kundi C. Timu hiyo ya Bafana bafana imefuzu Kombe la Dunia licha ya kuondolewa pointi tatu kwa kumchezesha mchezaji asiyestahili katika mechi za awali. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Afrika Kusini kushiriki Kombe la Dunia tangu ilipofuzu moja kwa moja kama mwenyeji mwaka 2010. Ushindi huo wa Afrika Kusini umeifanya Nigeria kumaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi hilo, na sasa italazimika kushiriki hatua ya mchujo ili kufuzu. Nigeria iliifunga Benin 4-0 nyumbani, baada ya mshambuliaji Victor Osimhen kufunga mabao matatu.