Home / News archive
News archive

This section shows archived news with its original publication dates. The article is displayed in its original language.

Afisa polisi wa Kenya afariki katika ajali ya barabarani Haiti

Maafisa polisi wanane wa Misheni ya Usaidizi ya Usalama wa Kimataifa (MSS) nchini Haiti wamejeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani Jumapili, huku afisa mmoja wa Kenya akifariki dunia. Kwa mujibu wa msemaji wa MSS, Jack Ombaka, tukio hilo lilitokea majira ya saa 11 jioni likihusisha magari mawili y...

NewstimeTR Haber Merkezi · · Updated 13/08/2026, 05:26:07
Afisa polisi wa Kenya afariki katika ajali ya barabarani Haiti
At a glance

Maafisa polisi wanane wa Misheni ya Usaidizi ya Usalama wa Kimataifa (MSS) nchini Haiti wamejeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani Jumapili, huku afisa mmoja wa Kenya akifariki dunia. Kwa mujibu wa msemaji wa MSS, Jack Ombaka, tukio hilo lilitokea majira ya saa 11 jioni likihusisha magari mawili y...

Maafisa polisi wanane wa Misheni ya Usaidizi ya Usalama wa Kimataifa (MSS) nchini Haiti wamejeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani Jumapili, huku afisa mmoja wa Kenya akifariki dunia. Kwa mujibu wa msemaji wa MSS, Jack Ombaka, tukio hilo lilitokea majira ya saa 11 jioni likihusisha magari mawili ya aina ya MaxxPro, ambapo gari moja lilipokuwa likivuta jingine lilipata hitilafu ya kiufundi. Maafisa waliojeruhiswa pamoja na raia walipelekwa katika Hospitali ya Lambert Santé iliyopo Pétion-Ville, ambapo afisa wa Kenya na raia mmoja walifariki dunia. “Maafisa wa polisi wanane wa MSS walijeruhiwa, wanne wakiwa katika hali mbaya hivyo wanahitaji kuhamishwa kwa ajili ya kupata matibabu maalum nchini Jamhuri ya Dominika baada ya kupokea huduma ya kwaza katika Hospitali ya Aspen Level 2,” alisema Ombaka katika taarifa yake. Aidha, Ombaka alitoa rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha baada ya tukio hilo.