Gida / Taskar labarai
Taskar labarai

Wannan sashe yana nuna tsoffin labarai da ranakun da aka wallafa su. An nuna labarin a harshensa na asali.

Ufaransa ‘yatupilia mbali’ kesi ya aliyekuwa mke wa Juvenal Habyarimana

Kulingana na mahakimu waliokuwa wanafuatilia kesi hiyo, hapakuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kumuhusisha na tukio hilo. Agathe Habyarimana alikuwa akihusishwa na kifo cha kiongozi huyo wa zamani wa Rwanda, kilichotokea Aprili 6, 1994. Mwanamama huyo, ambaye amekuwa akiishi nchini Ufaransa tok...

NewstimeTR Haber Merkezi · · An sabunta 2026-08-13, 05:26:24
Ufaransa ‘yatupilia mbali’ kesi ya aliyekuwa mke wa Juvenal Habyarimana
A taƙaice

Kulingana na mahakimu waliokuwa wanafuatilia kesi hiyo, hapakuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kumuhusisha na tukio hilo. Agathe Habyarimana alikuwa akihusishwa na kifo cha kiongozi huyo wa zamani wa Rwanda, kilichotokea Aprili 6, 1994. Mwanamama huyo, ambaye amekuwa akiishi nchini Ufaransa tok...

Kulingana na mahakimu waliokuwa wanafuatilia kesi hiyo, hapakuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kumuhusisha na tukio hilo. Agathe Habyarimana alikuwa akihusishwa na kifo cha kiongozi huyo wa zamani wa Rwanda, kilichotokea Aprili 6, 1994. Mwanamama huyo, ambaye amekuwa akiishi nchini Ufaransa toka mwaka 1998, aliikimbia Rwanda, siku chache baada ya kutunguliwa kwa ndege iliyokuwa imembeba mumewe, tukio lilopelekea kutokea kwa mauaji ya kimbari ambayo yalisababisha vifo vya watu 800,000 nchini humo. Uchunguzi kuhusiana na chanzo cha kifo cha Habyarimana ulianza toka mwaka 2008 baada ya taasisi moja ya Ufaransa kufungua mashitaka dhidi ya Agathe, ambaye pia alihojiwa baada ya kushukiwa kuwa sehemu ya jamii wa Wahutu ambao waliendesha mauaji dhidi ya Watutsi. Kulingana na mahakimu waliokuwa wanafuatilia kesi hiyo, hapakuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kumuhusisha na tukio hilo. "Ingawa taarifa bado zinaendelea kuzagaa, haziwezi kuwa na ushahidi wa kutosha," walisema mahakimu hao.